fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

apps Intaneti Maujanja Tanzania

Podcast ni nini? – Njia rahisi ya kusikiliza na kurusha vipindi kwa urahisi

tecno

Je umeshawahi kusikia kuhusu apps za Podcast? Je zina faida yeyote? Fahamu kuhusu njia hii rahisi ya kusikilizi vipindi utakavyo kwa muda uutakao, na pia njia ya kurusha vipindi vyako mwenyewe.

Huduma ya Podcast ni huduma ya bure inayowawezesha watu kupata kusikiliza huduma za kiredio kwa njia za intaneti katika mifumo kama vile mp3 na mingineyo ya sauti. Huduma hii ina waanganisha wasikilizaji na watengenezaji wa vipindi husika kwa njia rahisi ya huduma ya mtandao (intaneti).

Naweza Podcast

Naweza Show: Nje ya kurushwa kwenye redio, kipindi cha Naweza kinapatikana pia kwenye apps za Podcast

Historia ya jina Podcast; lilitengenezwa na Apple, likiwa muunganisho wa neno iPod (kifaa chao cha kwanza kwa ajili ya kusikiliza muziki) na neno broadcasting (urushaji matangazo)

Mafanikio ya huduma ya Podcast yaliletwa na Apple, ila kwa sasa utumiaji wake ni mpana zaidi. Kuna apps mbalimbali kwa ajili ya kompyuta na simu za aina zote zinazotoa huduma ya usikilizaji wa vipindi vya Podcast.

  • Msikilizaji: Utafungua app yeyote ya Podcast; Kama vile Google Podcast au kwenye apple app ya Podcast, utatafuta na kusikiliza vipindi au kufollow akaunti upendazo
  • Mrusha kipindi: Itakubidi utafute huduma za kuupload vipindi vyako, huduma za bure ni pamoja na Anchor FM.

Uzuri wa vipindi vya Podcast ni kwamba vinapatikana kwenye app yeyote ile ya kusikilizia vipindi vya Podcast. Apps zote zinafanya kazi za utafutaji wa mafaili spesheli ya Podcast kwenye mitandao mbalimbali kama vile mtandao wa Anchor FM na mingineyo.

Podcast ni podcast apps

Kuna apps mbalimbali kwa ajili ya kusikiliza vipindi vya Podcasts, uzuri vipindi ni vile vile. Unaweza kupenda app kutokana na utofauti wa muonekano au mapendekezo bora zaidi

Faida kuu:

  • Kuna vipindi vya vichekesho, vipindi vya miziki, vinavyoongelea filamu, vya kuelimisha na topics/masomo mengine mbalimbali.
  • Tofauti na redio ambapo lazima usikilizi kipindi flani muda flani kwenye Podcast hali ni tofauti, unaweza kuhifadhi episode na kusikiliza muda wowote utakaotaka, pia unaweza kusikiliza vipindi vya siku za nyuma kwa urahisi huo huo.
  • Kwa urushaji wa kipindi pia ni rahisi sana, na hili limewangulia njia watu kuanzisha vipindi vyao bila gharama kubwa au hadi kuajiriwa na redio stesheni. Kwa njia ya Podcast mtu yeyote mwenye ujuzi mdogo wa teknolojia anaweza kuanzisha kipindi chake.

Je kuna vipindi vya kitanzania vinavyopatikana kwenye mifumo ya Podcast?

Ndio, haraka haraka kuna akaunti mbili za kitanzania ninazozifuatilia kwa sasa.

  • Kipindi kuhusu maisha kinachokuja na stori za kweli kutoka kwa watanzania mbalimbali (Kiswahili) – Naweza Show
  • Kipindi kinachoendeshwa na wadada kadhaa kuzungumzia mambo mbalimbali yanayotokea au kutrend (Lugha ni kiswahili na kiingereza) – The Chai Podcast
SOMA PIA  Nani Mtawala Katika App Za Ku Chati Kwa Sasa?

Vipindi vingine maarufu ninavyofuatilia kupitia app ya Podcast ni pamoja vipindi vya uchambuzi wa ligi za mpira kama vile The Sky Sports Football Podcast, na ESPN FC Podcast.

Vipi je wewe tayari ni msikilizaji wa Podcasts? Tuambie huwa unasikiliza vipindi gani zaidi?

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania