Kama ulikuwa mfuatiliaji mzuri wa sakata la Bharti Airtel Tanzania pamoja na serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania utakumbuka vyema ile vuta ni kuvute zilizokuwepo kati ya pande hizo mbili.
Sote tunafahamu kuwa serikali inapata fedha za kuweza kujiendesha kutokana na kodi mbalimbali lakini pia ikiwa ni pamoja na kiwango cha hisa ambacho serikali inamiliki kwenye kamfuni/shirika fulani na baada ya muda fulani kuweza kupata gawio kisha pesa hizo kuingia serikalini (Wizara ya Fedha).
Kwa mujibu wa rais, Dkt. John Magufuli wakati wa tukio la ushuhuda wa ujio wa ndge mpya aliweza kuzungumzia kuhusu hisa ambazo serikali inamiliki kwenye kampuni ya mawasiliano, Airtel Tanzania. Huko nyuma serikali ya Tanzania ilikuwa ikimiliki asilimia arobaini za hisa (40%) huku upande wa pili huku upande wa pili wakimiliki 60%.
Katika njia ya kutafuta muafaka na serikali kuweza kupata gawio lao Bharti Airtel Tanzania wameamua kupunguza hisa zao kutoka 60 asilimia hadi 51% na hivyo kufanya hisa (umiliki wa kampuni ya Bharti Airtel Tanzania) upande wa serikali ya Tanzania kufikia 49%.

One Comment
Comments are closed.