Tayari simu janja zetu tunazitumia kama vitu mbalimbali mfano kama kalenda, kifaa cha kusomea vitabu, tochi, kununua na kutuma pesa, rimoti na sasa kupitia Keyfree utaweza itumia kama funguo ya gari yako.
Kampuni kutoka Canada Keyfree Technologies wamechukua hatua katika teknolojia kwa kuleta kile kinachoitwa “digital car key solution,” (Maana: Ufumbuzi wa gari kidigitali).
Wamefanya hili kwa kuweka funguo za gari katika simu janja. kampuni hii ilionyesha/tangaza bidhaa yake hii katika CES 2015 (Consumer Electronics Show 2015). Kazi ya Keyfree ni kubadilisha mfumo mzima wa namna ya kufanya zile kazi zote ambazo ufunguo wa gari ulikua unafanya (kufunga, kufungua, kuweka na kutoa loki). Badala ya kutembea na funguo sasa utahitaji kutembea na simu janja yako tuu.
App katika simu yako (keyfree) itawasiliana na gari kupitia Bluetooth ili kufikisha mawasiliano na kuweza kulipa gari amri. Ukifika karibu na gari lako tuu gari lita sensi (kutokana na Bluetooth) na kuweza kujitoa loki. Mfumo wa Starter ya gari utakuwa wa aina ya Push to start (Ule wa kubofya ili kuwasha) ambao utahitaji installation (ufungaji)
Kampuni hiyo inadai kuwa huo mfumo mzima wa kutumia simu kama ufunguo wa gari una usalama wa daraja ya kijeshi (millitary grade security). Watumiaji wanaweza sambaza funguo hizo za kidigitali na familia na marafiki wanaotumia hiyo App. Mmiliki wa hilo gari anaweza Kufuta zile funguo za kidigitali kwa marafiki au familia pale anapoamua na watu hao hawataweza tena kufungua gari hilo.
Pia mwenye gari anaweza fuatilia nyendo za gari yake na kujua nani kaendesha au alikua nayo mda flani kwa kuangalia nani alitumia funguo (katika orodha ya wale ndugu na jamaa waliopewa funguo)
Mfumo mzima wa KeyFree unagharimu dola za kimarekani ($) 199 pamoja na garama za ufungaji (installation). Mfumo huu wa funguo utakuwa mzuri zaidi kwa watu kadhaa wanaotumia gari moja fikiria kitu kama yale magari ya kukodishwa au hata ya makampuni mbali mbali ambayo hayana dereva mmoja wa kudumu.
Wazo lako ni muhimu, ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram
[ConsumerReports.org]
No Comment! Be the first one.