fbpx
apps, Facebook, Intaneti

Facebook Messenger kuwa ndogo zaidi na mambo mapya yapo njiani. #Apps

facebook-messenger-kuwa-ndogo-zaidi
Sambaza

App ya Messenger kuwa ndogo zaidi hivi karibuni. Baada ya miaka mingi ya app hii kuzidi kuongezeka ukubwa na utumiaji wa chaji kwenye simu, Facebook wamesema ipo njiani kuwa ndogo zaidi na kupata mambo mapya.

Kampuni hiyo inayomiliki apps mbalimbali za kijamii imesema ya kwamba app ya Facebook kuwa ndogo zaidi katika matoleo yayokuja hivi karibani.

Facebook Messenger kuwa ndogo zaidi
Facebook Messenger kuwa ndogo zaidi: Kuna mambo mengi mapya yapo njiani, hii ni kulingana na Mark Zuckerberg alipokuwa akielezea kwenye mkutano wa Facebook wa kila mwaka wa Facebook F8.

Facebook wamesema wanafanyia kazi toleo litakalokuwa na ukubwa wa MB 30 tuu, hii ni takribani asilimia 20 ya wastani wa toleo la sasa la app hiyo. Mfano kwenye simu yangu ya Samsung Galaxy Note 8 kwa sasa app hiyo inachukua zaidi ya MB 260 ya data.

INAYOHUSIANA  Idadi ya watumiaji wa Intaneti yaongezeka Ulimwenguni

Katika uamuzi wao Facebook wamesema wanatengeneza toleo jipya kiupya kabisa kuanzia mwanzo, na wana lengo toleo jipya la app hiyo kuweza kufunguka ndani ya sekundi 2 au chini pale ikifunguliwa. Kwa kuanzia toleo jipya litaanza kupatikana kwa watumiaji wa iOS na si Android, tunadhani kipaumbele hakijapewa kwa watumiaji wa Android kwa sababu tayari kuna toleo la Messenger Lite ambalo ni dogo – hili halikuwa linapatikana kwa watumiaji wa iPhone.

INAYOHUSIANA  Smart Reply: Gmail Kuja na Majibu kwa Ajili ya Barua Pepe Zako

Mengine mapya yanayokuja;

Sehemu rasmi kwa ajili ya marafiki wa karibu na ndugu.

  • Facebook wanafanyia kazi sehemu mpya ndani ya app ya Messenger itakayohakakikisha watumiaji wake wanapata eneo rasmi la kuangalia status na kushare mambo na marafiki wa karibu pamoja na ndugu.
  • Sehemu hii itamuwezesha mtumiaji kualika ndugu na marafiki katika utazamaji wa video. Kwa video hizo mtaweza kupata eneo spesheli la kuchati wakati mnatazama.
INAYOHUSIANA  AzamTV App yapakuliwa zaidi ya mara milioni moja
Facebook Messenger app kwa ajili ya kompyuta
Facebook Messenger app kwa ajili ya kompyuta: Mac na Windows

Pia toleo la Messenger kwa ajili ya kompyuta, Windows na Mac, lipo njiani kuja muda wowote kuanzia sasa.

Je wewe ni mtumiaji wa app ya Messenger? Una mtazamo gani juu ya ukubwa wake na utumiaji wake wa intaneti?

Utafiti: Hizi ndio Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi katika simu za Android 

Vyanzo: TheVerge na mitandao mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |