fbpx
Snapchat

Licha Ya Corona Snapchat Imekua Kupitia Mauzo Na Utazamwaji!

snapchat-kukua-kimauzo-na-utazamwaji
Sambaza

Snapchat ni mtandao wa kijamii ambao ulikuja kwa kasi sana, ukiachana na ujuo wake huo bado ilianza kushuka kwa haraka ikawa kinyume cha watu walivyodhania. Kabla ya isntagram, WhatsApp na Facebook hazijaja na huduma ya ‘Stories’ Snapchat ndio ilikua inashika usukani.

Ni wazi mapato na watumaiji wa snapchat walishuka kwa kiasi kikubwa tuu maana wengi waliona hakuna haja sana ya kuingia katika mtandao huo (ambao umeingia) kwani vitu vingi ambavyo vipo katika mtandao bado vipo katika mitandao mingine ambayo watumiaji hao hao walikua wanaitumia tokea zamani.

INAYOHUSIANA  Snapchat kuleta selfie za 3D baada ya kununua Seene
Muonekano wa sehemu zote za app hiyo

Ukiachana na yote hayo bado mtandao wa Snapchat haukati tamaa, imekua ikizidi kujiboresha kwa kuongeza vipengele vingi tuu ili kuhakikisha kuwa wanabaki katika ushindani wa kimitandao ya kijamii.

Ni wazi kuwa virusi vya Corona vimeharibu hali ya hewa sana maana kila bishara ambayo ilikua inafanya vizuri haifanyi vizuri tena licha ya kukiwa na zile chache ambazo zimejipatia soko kubwa kupitia janga hili.

INAYOHUSIANA  Maelfu ya watumiaji wa app ya SnapChat hawajapendezwa na sasisho jipya

Ni wazi kwa huduma kama za kimitandao ya kijamii kukua kwa watumiaji kwa kiasi kwani katika kipindi cha janga hili ni wengi wantumia mitandao ya kijamii kuwasiliana.

Kwa snapchati kupitia robo ya mwaka huu (2020) imekua na taarifa nzuri maana watumiaji wameongezeka katika mtandao huo na pia mapato yameongezeka kwa kiasi kikubwa na hili ni ukilinganisha na robo ya kwanza ya mwaka jana.

INAYOHUSIANA  Snapchat Kuleta 'Link' Na 'Background' Katika Stories!

Niandikie hapo chini katika uwanja wa maoni je wewe unaona ni mwendeleo mzuri wa Snapchat? Je vipi kama janga la corono likitokomea bado unadhani wataweza kukua tena? Usisahau kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Na Wewe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags:

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com