fbpx
Facebook, Intaneti, Mtandao wa Kijamii, Snapchat, Teknolojia

Matumizi ya mitandao ya kijamii huchochea upweke! #Utafiti

matumizi-ya-mitandao-ya-kijamii-huchochea-upweke
Sambaza

Tangu mitandao ya kijamii itambulishwe imekuwa sehemu kubwa katika kuleta mabadiliko katika maisha ya kila siku. Ni wazi kuwa watu hutembelea mitandao ya kijamii mara kwa mara.

Katika utafiti uliofanywa na wanasaikolojia umebaini kuwa mitandao ya mawasiliano ya kijamii kama vile Twitter, Facebook na Instagram inasababisha watu wengi zaidi kuJIhisi wenye upweke na kubainisha kuwa kwa saa zaidi ya mbili ya matumizi ya mitandao ya kijamii kwa siku huongeza uwezekano mara dufu wa mtu kujihisi ametengwa na jamii.

Wanasaikolojia wanasema matatizo ya afya ya akili na kutengwa na jamii yamefikia katika viwango vya mlipuko kwa vijana.

Katika utafiti uliofanywa na watafiti wa chuo kikuu cha Pittsburgh, uliohusisha watu takribani 1,787 wenye umri kati ya miaka 19-32 ambao hutembelea mitandao ya kijamii kama Facebook, YouTube, Twitter, Google Plus, Instagram, Snapchat, Reddit, Tumblr, Pintrest, Vine na LinkedIn. Imeonekana  kuwa kwa wale wanaotembelea mitandao ya kijamii mara 58 au zaidi kwa wiki wapo kwenye hatari mara 3 zaidi ya kujihisi kama wametegwa kwenye jamii kuliko wale ambao hutembelea mitandao ya kijamii chini ya mara 58 kwa wiki.

Matumizi ya mitandao ya kijamii kwa muda wa saa 2 au zaidi kunaongeza nafasi ya mtu kujihisi kama ametengwa/mpweke.

Matumizi ya mitandao ya mawasiliano ya kijamii pia yanaweza kusababisha hisia za kutengwa, kama vile kuona picha za marafiki zako wakifurahia tukio fulani ambalo wewe hukualikwa na mpaka hivi sasa bado hawajabaini kipi kilianza kati ya matumizi ya mitandao ya kijamii au matatizo ya kuhisi kutengwa.

INAYOHUSIANA  Undani wa toleo jipya la Android 9 Pie

Wengine wanajiuliza ‘Je ni mitandao ya kijamii ndiyo inasababisha upweke huo au tuu ni kwamba watumiaji wa mitandao ya kijamii tayari ni wapweke na wanaona mitandao hiyo kama sehemu ya kupata nafuu ya upweke huo… Wewe unaonaje hapa?

Mitandao ya kijamii imerahisisha katika ufikishaji wa taarifa kwa haraka zaidi sana. Je, wewe unatembelea mitandao ya kijamii mara ngapi kwa siku?

 Vyanzo: News Sky, Lifehacker, BBC

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|