fbpx
Apple, apps, iOS

Apple Music: Huduma ya app ya Muziki ya Apple yapatikana Kwa Android na iOS

apple-music-app-ya-muziki-ya-apple-yapatikana-kwa-android-na-ios
Sambaza

Huduma ya app ya Muziki ya Apple yaanza kupatikana rasmi. Apple imewezesha rasmi utumiaji wa huduma yake ya muziki kupitia app ya Apple Music.

Kikubwa zaidi ni kufanikisha uwezo wa kutumia app hiyo Kwa watumiaji wa Android pia. Kawaida huduma zao nyingi huwa zinapatikana kwa watumiaji wa simu za iOS, yaani iPhone tuu.

app ya Muziki ya Apple
App ya Muziki ya Apple, inayokwenda kwa jina la Apple Music

Uamuzi wa kuwezesha huduma hiyo Hadi kwa watumiaji wa Android inaonesha kwa kiasi gani Apple wanataka kuleta ushindani kwa huduma zingine kama vile Boomplay, Deezer na Spotify. Kwenye gharama bado Boomplay ni huduma nafuu, takribani Tsh 3,000 kwa mwezi wakati Apple Music ni takribani mara mbili ya hii.

INAYOHUSIANA  Jamaa Avunja Vunja iPhone Na Mac Katika Apple Store Huko Ufaransa!

Malipo?

Huduma imeanza kupatikana bure kwa miezi 6 ya kwanza kisha kupanda hadi kufikia takribani TSH 6,900/= kwa mwezi kwa mtumiaji mmoja na kwa TSH 10,900/= pekee kwa akaunti ya watu wengi (familia) – hii inaweza wezesha hadi watu 6 kutumia akaunti tofauti lakini zenye kulipiwa na kadi moja ya benki. Ni nzuri kwa watu mnaoaminiana, kama vile wanafamilia.

Je unataka kujaribu app hii? Utakachotakiwa ni kuwa na akaunti ya Apple ID, kama hauna basi itakuchukua dakika chache kutengeneza fuata linki hizi chini.
Apple ID (kuandikisha) – Apple/Apple ID

INAYOHUSIANA  Podcast ni nini? - Njia rahisi ya kusikiliza na kurusha vipindi kwa urahisi

Download Apple (Android) – Google Play store | AppStore (iOS)

Ujio huu umeambatana pia na uamuzi wa Apple wa kuziwezesha huduma zake zingine kama vile iCloud na Appstore kuweza kupatikana katika mataifa na maeneo 20 mengine mapya, soma zaidi hapa -> Teknokona/ Huduma za Kampuni ya Apple kufikia Nchi nyingi sasa ikiwemo Tanzania

Je una mtazamo gani juu ya huduma ya Apple Music ukilinganisha na huduma tulizozizoea kama vile Boomplay? Je unalipia huduma yeyote ya Mziki?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |