fbpx

Apple, Samsung, Teknolojia

Apple Vs Samsung: Tunatoa Mwaka (2020) Kwa Apple!

apple-vs-samsung-kwa-mwaka-2020

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Apple na Samsung wamekua wakichuana vikali sana katika soko la kutengeneza na kuuza simu. Ni sawa iko wazi wengi wetu tunapenda samsung, lakini kwa mwaka 2020 inabidi Apple ipewe heshima yake.

Ilikua imezoeleka sana kwa kampuni ya Apple kutoa simu moja kila mwaka mwezi wa tisa mara nyingi. Kwa mwaka huu wametoa simu mbili katika nyakati tofauti tofauti kabisa.

Kumbuka mwezi wa nne walitoa iPhone SE(2020) na mwezi wa kumi wakatoa simu ne yaani iPhone 12, iPhone 12 Mini, iPhone 12 Pro na iPhone 12 Pro Max.

iphone 12
iPhone 12 ikiwa na iPhone 12 Mini

Kwa mara ya kwanza ndio Apple wameweka utofauti katika simu zake za kawadia (iPhone 12 Pro) na zile kubwa zake (iPhone 12 Pro max) ambapo zamani simu zilikua zinatofautiana ukubwa tuu lakini sifa zake zilikua zinafanana tuu

Pengine huu ndio mwaka ambao kampuni imezindua na kutangaza vifaa vingi zaidi kuliko miaka yake mingine yote kwa harakaharaka  mwaka huu wameachia simu tano, iPad Pro, Airpods, Airpods Pro (ambazo zinafunika kichwa), OS 14 (Mpya) n.k

SOMA PIA  OS Fuchsia Inaweza Kuwa Mbadala Wa Android Kutoka Google!

Ukiachana na hayo yote bado vyanzo mbalimbali vya habari za kiteknolojia vimetoa orodha ya simu janja nzuri zaidi kwa mwaka 2020, iPhone 12 inashikilia namba moja ukilinganisha na simu zingine.

Ukiachana na vitu ambavyo Apple imefanya kwa mwaka 2020 hii haimaanishi kuwa Samsung hawajafanya lolote… unakumbuka zile simu tatu S20, S20+ and S20 Ultra zote zilitoka mwaka huu na zimefanya vizuri sana.

SOMA PIA  Jua Umefanya Nini Leo Mwaka Jana Na TimeHop - #App
Samsung S20, S20+ Na S20 Ultra
Samsung S20, S20+ Na S20 Ultra

Je kwa mwaka 2021 unafikiri simu zitakazo toka kwa makampuni haya mawili zitakuaje? unafikiri ni nani atamkimbiza  mwezake? ningependa kusikia kutoka kwako niandikie hapo chini katika uwanja wa maoni

Kumbuka kutembelea mtandao wako pendwa wa Teknokona kila siku kwani daima tupo nawe katika teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza
Tags: ,

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

    Toa Maoni

    Your email address will not be published. Required fields are marked*