Ndio hili linaweza likawa linawashtua wengi na kuwa na maswali kibao maana tumeona WhatsApp ikiwa inapatikana mpaka kwenye kompyuta vipi kuhusu iPad?
Kumbuka mwanzo kabisa WhatsApp ilianzishwa mahususi kwa ajili ya matumizi katika vifaa vya simu lakini kwa sasa Apple wamesema ipenye mpaka kwenye iPad.
Kwa sasa kuna toleo la majaribio ambalo liko katika hatua za majaribio, hii inaonyesha dhahiri kwamba hili wamelipa nguvu sana ndio maana limefikia katika hatua hii.
Mwanzoni ni wazi kwamba watumiaji wa WhatsApp walikua wanatakiwa kutumia ile WhatsApp Web ili kuweza kupata huduma hiyo.
Vyanzo mbalimbali vinaweka wazi kwamba hata toleo hili la iPad likitoka ni kwamba halitakua na tofauti kubwa sana na toleo lile la App ya Mac.
App hiyo ikishakua imepakuliwa katika iPad basi kama kawaida kwa kutumia QR Code utaweza hamisha mawasiliano katika WhatsApp yako ya simu na mazungumzo kufikia katika iPad hiyo.
App hiyo inaweza kufanya kazi hata kama simu ikiwa mbali na iPad hiyo cha muhimu ni kuhakikisha kwamba iPad hiyo inapata intaneti —-hata kwa kutumia WiFi.
Kwa haraka haraka hapa unaweza ona kwamba App hii kwa ajili ya iPad haina tofauti sana na ile App ya kompyuta utagundua tuu ni app mwenza kwa WhatsApp ya simu (companion App).
Hapa cha msingi ni kwamba hata watumiaji wa iPad inabidi washukuru tuu kwamba wameweza kupata App kwa ajili ya vifaa vyao sio?
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je unadhani ni sawa kwa WhatsApp kuingia katika iPad kwa kipindi hiki?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.