Kampuni ya Samsung inategemewa kuanza uzalishaji wa paneli za OLED kwa ajili ya matoleo yajayo ya iPhone mnamo robo ijayo ya mwaka. Samsung inategemewa kuzalisha kiasi cha paneli milioni themanini (80) kwa ajili ya matoleo yote ya iPhone 14 ambayo ni iPhone 14, iPhone 14 Max, iPhone 14 Pro na iPhone 14 Pro Max.
Mgawanyo wa paneli hizo unatarajiwa kuwa; paneli milioni thelathini na nane (38) kwa ajili ya iPhone 14 na iPhone 14 Max huku milioni arobaini na mbili (42) zikiwa kwa ajili ya iPhone 14 Pro na iPhone 14 Pro Max.
Awali, kampuni ya Samsung ilitazamiwa kutengeneza paneli kwa ajili ya matoleo ya iPhone 14 ya juu tu, ambayo ni Pro na Pro Max, huku paneli za matoleo yaliyobaki yakitarajiwa kutoka kwa kampuni za LG na BOE. Lakini, hivi karibuni pametokea mzozano baina ya kampuni ya Apple na BOE, juu ya namna ya utengenezaji wa paneli hizo, kampuni ya Apple ikisemwa kutoridhishwa na mabadiliko yaliyofanywa na BOE katika utengenezaji.
Kampuni ya Apple itakuwa ikitathmini tena paneli kutoka kampuni ya BOE wiki inayokuja. Suala hili limesababisha Samsung kupata tenda hio pia, kwa kuwa ndio kampuni yenye uwezo mkubwa wa kutengeneza paneli za OLED kwa wingi, na ubora kati ya kampuni hizo tatu.
Chanzo: Gadgets360
No Comment! Be the first one.