fbpx
Microsoft

Jinsi Ya Kutumia Microsoft Office Bure! #Online

tumia-microsoft-office-bure
Sambaza

Kwa kawaida Microsoft office huwa inauzwa kwa dola za kimarekani 70 kwa mwaka. Ni huduma ya kulipia kila baada ya muda Fulani.. yaani unapewa leseni ya kutumia ndani ya muda Fulani kisha unalipia tena ili kuendelea kutumia.

Microsoft Office ina program muhimu sana katika maisha ya kila siku. Leo TeknoKona inakuonyesha jinsi ya kupata Word, Excel, PowerPoint, na application zingine za Microsoft bila hata kulipia thumni.

INAYOHUSIANA  PlayStation 4 Neo: Ujio wa toleo jipya la PS4 mbioni
Microsoft Word Katika Mtandao

Haitajalisha unatumia kompyuyta gani iwe PC ya windows 10 au hata Chromebook una uwezo wa kutumia Microsoft office ukiwa katika mtandao. Kwa kifupi huduma hii itakulazimu uwe katika mtandao ndio uitumie.

Kutumia kompyuta yako ingia katika mtandao wa Office.Com na kisha jiunge kwa ku ‘Sign In’ kwa kutumia akaunti ya Microsoft (kama huna, tengeneza).

Ukishaingia ndani click alama za Word, Excel, au PowerPoint ili kuanza kutumia. Kumbuka huduma hizi hazitaweza fanya kazi kama hakutakuwa na huduma ya kimtandao (intaneti). Kumbuka ukitumia kwa muundo huu kila kitu kinakuwa ni bure kabisaa…

INAYOHUSIANA  Bidhaa 10 za Microsoft Ambazo Pengine Huzifahamu

Niambie je njia hii ulikua unaijua? Niandikie hapo chini katika boksi la maoni. Pia usisite kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwa habari mbali mbali za kiteknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com