fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Realme simu Teknolojia

Yafahamu ya muhimu kuhusu simu janja Realme Narzo 30 5G #Uchambuzi

Yafahamu ya muhimu kuhusu simu janja Realme Narzo 30 5G #Uchambuzi

Spread the love

Oppo ndio kampuni inayobeba simu janja zenye jina “Realme” ambazo zimeshatoka nyingi tuu sokoni na si kama wamekomea hapo kwani mnamo Mei 26 ya mwaka huu imezinduliwa Realme Narzo 30 5G.

Makampuni mengi yameendelea kutoa simu janja za 5G ambazo kwa idadi zipo nyingi sokoni na washindani kibiashara wanajitahidi kuileta teknolojia hiyo ,machoni pa watu. Realme Narzo 30 5G ni rununu ambayo imezinduliwa siku chache zilizopita na sifa zake ni:

SOMA PIA  Sarafu: App ya Azam inayomrahisishia mteja kununua bidhaa na kufikishiwa mpaka alipo bure

Ubora wa kioo|Kipuri mama

Simu hii ina kioo chenye urefu wa inchi 6.5, ubora wake ukiwa ni IPS LCD, ung’avu wa hali ya juu halikadhalika upande wa kipuri mama pia ni yenye uwezo hasa ukizingatia ni rununu iliyo na kasi ya 5G. Hapa nazungumzia Dimensity 700 inayotengenzwa na MediaTek.

Memori|Kamera

Kivutio cha watumiaji wengi wa simu janja ni ukubwa wa diski uhifasdhi kuanzia ile inayohifahi vitu kwa muda mfupi (RAM) hadi ile inayotunza mpaka unapoamua kupunguza vitu vilivyomo kwenye rununu. Simu hii ina RAM GB 4, diski uhifadhi GB 128 lakini pia inawezekana kuweka memori ya ziada. Ina kamera 3 nyuma-MP 48 na mbili zina MP 2, mbele kuna kamera moja yenye MP 16.

Kamera ya nyuma/mbele zina uwezo wa kurekodi picha jongefu za ubora wa 1080px. Halikadhalika kuna taa ya kuongeza mwangaza kwenye kamera ya nyuma.

Uwezo wa betri|Mengineyo

Uwezo wa betri kwenye simu hii tunazungumzia 5000mAh, 18W kwenye upande wa teknolojia ya kuchaji haraka na si la kutoka na kuweka. Ule waya wa kuchajia lazima uwe ni USB-C 2.0, USB On The Go (OTG), ina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, WiFi, inatumia kadi mbili za simu, Bluetooth 5.1, teknolojia ya kutumia alama ya kidole imewekwa kwa pembeni kwenye kiutufe cha kuzima/kuwasha simu.

Inapatikana katika rangi ya Fedha na Bluu. Bei yake ni karibu $267|zaidi ya Tsh. 614,100.

Simu hii inatazamiwa kuingia sokoni mwezi Juni na bei iliyopo ile ya ughaibuni. Tunakaribisha maoni yako kuhusu uchambuzi wa simu hii na daima usiache kutufuatilia.

Vyanzo: GSMArena, Gadgets 360

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania