Unakumbuka kuna kipindi Huawei ilikua iko juu sana? ilikua ikichuana vikali na makampuni mengine makubwa kama vile Apple na Samsung.
Kampuni ilikuja kuporomoka katika soko la kuuza na kutengeneza simu janja, moja kati ya sababu iliyopelekea hivyo ni mwaka 2019 ya raisi wa zamani wa marekani bwana, Donald Trump….
…kuiwekea kampuni hiyo baadhi ya vikwazo vya kufanya biashara katika taifa hilo, hali ambayo ilifanya kampuni kokosa soko huku na kufeli katika madili mengine.
SOMA ZAIDI KUHUSU HUAWEI –> HAPA <–
Sasa unaweza ukaanza kujiuliza kwamba hao Huawei wana mkakati gani ambao utawasaidia ili angalau wafike hata katika tano bora ya soko la wauzaji na watengenezaji wa simu?

Kwa haraka haraka ni kwamba Huawei wana teknolojia kubwa sana lakini kinachohisiwa na watu wengi wanchodai ni kwamba wanabaniwa katika soko.
Wadai vitu vizuri wanavyo, teknolojia wanayo..ila ni figisu tuu ndio imeingilia kati..
Kumbuka baada ya Huawei kuanza kupata majanga haya waliamua hata kuuza nembo yao maarufu ya simu inayojuliana kama Honor……
…..hii ikiwa inamaanisha kuwa Huawei hawawezi tena kutengeneza simu huku wanatumia jina hilo la Honor

Mwenyekiti wa kampuni ya Huawei bwana Guo Ping, amehakikishia watu kuwa kampuni hiyo bado inafnaya juu chini katika kuhakikisha kuwa inarudi katika soko
Na ujio wake yenyewe itakua inajikita sana katika kuhakikisha kuwa inapata nafasi yake ile ile ambayo ilikua ina tamba nayo mwanzo.
No Comment! Be the first one.