Katika mipango ambayo Huawei ipo nayo kwa sasa ni kutoa simu janja yenye kamera ya mbele iliyojificha jambo ambalo linadhihirika kutokana na kwenda kupata idhibati ya mchoro wao unaoonyesha muonekano mzima wa simu janja.
Mpaka sasa ni ZTE tu ndio ambao wameshatoa simu janja ambayo kamera ya mbele imejificha ambapo pia wanatazamiwa kutoa toleo la pli katika siku za usoni. Teknolojia hiyo inaonekana kuvutia makapuni kadhaa ambapo Samsung kupitia rununu Fold 3 huenda ikawa na muundo huo wa kamera halikadhalika Oppo.
Kwa mujibu wa mchoro huo simu janja husika inawezekana ikawa ni ya uwezo wa kati kwa maana ya kwamba uwezo wake hautakuwa ni wa juu sana lakini kwa jicho la haraka haraka tuu inavutia!.

Ni vigumu kusema mchoro huo unafanana na simu janja gani ya Huawei lakini mbali na ambayo vimeshafamika kwa kiasi ambacho kinamfanya mteja wa awe na shauku ya kuona bidhaa kamili.
Mambo ndio hivyo yameshaingia jikoni na pengine simu janja hii ikapata wateja wengi duniani hasa ukizingatia teknolojia inakua kila uchwao halikaadhalika na mahitaji ya simu janja nayo yanazungumzika.
Kwa muhktadha huo hatuna budi kusubiri na kuweza kufahamu kwa kina kuhususifa za bidhaa husika. TeknoKona tunasema “Kaa nasi”.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.