fbpx

Simu ya kamera MP 64 na MP 100 ipo njiani kuja

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Tulianza na kamera za ubora wa lai ya nchini lakini katika miaka ya karibuni kamera za kwenye simu janjazimekuwa zikionekana kuwa bora na hivyo basi kutoa picha zenye muonekano wa hali ya juu. Rununu za namna hiyo zipo nyingi katika miaka ya hivi karibuni na kwa mwaka 2019 tutegemee kuona MP 64 na MP 100 kwenye kamera ya rununu.

kama mtu ambae huwa napenda simu janja ambayo ina kamera inayotoa picha zenye ubora wa hali ya juu huwa ni vigumu sana kutoweza kuzungumzia habari ambazo ni nzuri kwa wana teknolojia. Qualcomm wanafahamika sana kwa utengenezaji wa vipuri mama vya matoleo mablimbali kama 660, 670, 675, 710, 845, 855 na ubora wa juu kabisa kwenye kamera mpaka sasa unabeba jumla ya MP 48 kwa maana ya kwamba kamera nne (4) na kila moja ikiwa na MP 12.

INAYOHUSIANA  App 6 Bora Za Kamera Kwa Ajili Vifaa Vya Android!

Mwaka 2019 tutarajia kuingia sokoni kwa simu janja ambayo ina MP 64 na nyingine ikiwa na MP 100 kwa ujumla!. Hii inamaanisha kuwa simu hizo huenda zikawa na kamera ambazo zina MP 16 au MP 25. Kitu hicho kinachagizwa kwa sana na uwepo wa Xiaomi Mi 9 na Redmi Note 7 Pro ambazo zina MP 48 kamera kuu lakini hata vivo V15 Pro ina MP 48 kamera ya mbele na MP 32-kamera ya nyuma.

Simu ya kamera

Ubora wa kamera aambayo kipuri mama kwenye simu husika ni Qualcomm.

Teknolojia ya kamera ndio hivyo inaendelea kukua kila inapoitwa leo na wewe kama ni mpenzi wa simu rununu basi inabidi ujipange kununua rununu ya namna hiyo.

Vyanzo: GSMArena, Digital Camera World

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.