fbpx
Huawei, Operating System

Huawei wana programu endeshaji (OS) yao kwa ajili ya simu na kompyuta

huawei-wana-programu-endeshaji-os
Sambaza

Kampuni ya Huawei wana programu endeshaji (OS) yao kwa ajili ya simu na kompyuta, haya yamesemwa na msemaji wao mkuu.

Wamefanya uamuzi wa kutengeneza progamu endeshaji yao kwa ajili ya sababu za kiusalama kama ikitokea wakajikuta hawawezi kutumia Android kwa simu au Windows kwenye kompyuta wanazotengeneza.

Hatua imechukuliwa kutokana na hali mbaya kimahusiano kati ya shirika hilo na serikali ya Marekani. Mfano tayari kampuni nyingine ya kichina – ZTE, ilipigwa marufuku na kuwekewa vikwazo kutotumia teknolojia za Marekani. Uamuzi huo dhidi ya ZTE ulimaanisha kampuni hiyo ikashindwa kutumia tena Android na Windows na suala hili likawaaribia sana kibiashara.

INAYOHUSIANA  Huawei yajigamba na Kirin 980

Kampuni ya Huawei imesema imetengeneza tayari programu endeshaji yao ili kujilinda kama uamuzi kama huo ukaja kufanywa dhidi yao.

Huawei wana programu endeshaji ya kwao
Huawei wana programu endeshaji ya kwao : Kwa kiasi kikubwa Huawei imekuwa kampuni kubwa sana kwenye teknolojia za mawasiliano kwa sasa, Huawei ni moja kati ya makampuni makubwa matatu ya juu sokoni kwenye bidhaa za simu; likiwa linashindana moja kwa moja na Apple katika kushika nafasi ya pili

Ila kwa sasa wataendelea kutengeneza bidhaa na kutumia programu endeshaji za Android na Windows.

Serikali ya Marekani inadai kampuni ya Huawei inatumia teknolojia za udukuzi kwenye bidhaa zake ili kuisaidia kijasusi serikali ya China, Huawei wameendelea kukataa madai haya. Huawei wamesima uamuzi huu ni wa kisaisa zaidi na pia ni kwa kuwa Marekani inaogopa ukuaji wa kasi wa shirika hilo kwenye teknolojia kama ya 5G n.k, kwani hii inamaanisha mashirika ya kijasusi ya Marekani yatashindwa kudukua mataifa yanayotumia teknolojia za Huawei.

INAYOHUSIANA  Honor 10 Lite ni nusu ya mtangulizi wake

Soma pia – Marekani wazidi kuibana Huawei, teknolojia ya 5G inaweza ikawaokoa kimauzo

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |