fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Asus simu

Qualcomm Kuja Na Simu Janja Yake Kwa Ushirika Wa Asus!

Qualcomm Kuja Na Simu Janja Yake Kwa Ushirika Wa Asus!

Spread the love

Qualcomm ni kampuni kubwa sana inajihusisha na maswala mengi ya teknolojia ikiwemo kuuza baadhi ya vipuri kwa makampuni makubwa kama vile Apple.

Kwa kuwa teknolojia ya simu inakua kwa kasi sana siku hizi basi Qualcomm na yenyewe imeona isisubiri sana imeona kwamba isisubiri ije na simu janja yake.

Simu Janja Kutoka Qualcomm Na Assus

Simu Janja Kutoka Qualcomm Na Assus

Kampuni imeamua kushirikiana na kampuni ya Asus na kwa kuanzia wanadai simu hii itaanza kupatikana katika nchi za China, Ujerumani, Ulaya na Marekani.

Mpaka sasa jina la simu janja hii bado halijawekwa wazi lakini makampuni yote mawili yanadai kuwa itakua ya kimapinduzi zaidi. Vyanzo vingine vinasema itaitwa SNAPDRAGON

Kingine ni kwamba Asus wao kwa kiasi kikubwa sana wamehusika na maswala ya ‘Hardware’ huku  Qualcomm wakihusika zaidi na ‘Software’

SOMA PIA  Jelly: Simu janja ndogo zaidi, ya kutosha kiganjani inayokuja na mfumo wa 4G

Sifa Zake Kwa Uchache Ni

Inakuja na Inchi 6.78, 144Hz Samsung OLED panel, Ujazo uhifadhi wa GB 512, RAM ya GB 16GB, senya ya alama za vidole (fingerprint), Uwezo wa  5G.

Inakuja na uwezo wa betri wa 4,000mAh huku ikiwa inakuja na Os ya Android 11.

Kama simu nyingi zinavyokuja siku hizi na simu hii itakuja na kamera tatu kutoka megapixel 64, 12MP mpaka 8MP huku zote zikiwa zina uwezo tofauti katika kupiga picha na kuchukua video.

SOMA PIA  BlackBerry Haijafikia Malengo Yake, Je Huu Mwisho Wa Simu Zake?

Kamara ya mbele itakua na MP 24.

Simu Janja Kutoka Qualcomm Na Assus

Simu Janja Kutoka Qualcomm Na Assus

Simu inatarajiwa kwa mara ya kwanza kuanza kupatika mwezi agosti mwaka huu. kumbuka jina bado haliko wazi moja kwa moja!

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Diama Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania