fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Huawei Teknolojia

Vifaa milioni 100 kutumia HarmonyOS mwaka huu, Huawei.

Vifaa milioni 100 kutumia HarmonyOS mwaka huu, Huawei.

Huawei wasema wanategemea vifaa milioni 100 kutumia HarmonyOS kufikia mwisho wa mwaka huu. HarmonyOS ni programu endeshaji inayolenga kuleta ushindani kwa Android.

milioni 100 kutumia HarmonyOS

Lengo la kupata vifaa milioni 100 kutumia HarmonyOS ni la chini, bado wanategemea mambo yakienda vizuri basi viwe vifaa milioni 300

 

Makamu wa Rais wa Huawei, Bwana Xu Zhijun amesema kinachofanyika kwa sasa ni maboresho zaidi ya jinsi programu endeshaji hiyo inatambua na kufanya kazi kwa ufanisi kwenye vifaa vya elektroniki vya aina tofauti tofauti. Ni lengo la Huawei kuiwezesha programu endeshaji hii kutumika kwenye vifaa vingi tofauti kama vile Televesheni janja, simu janja, saa janja, na vifaa vingine mbalimbali vya elektroniki vya kisasa.

SOMA PIA  Oparesheni ya kuunganisha sehemu za siri za watu tofauti yafanyika! #Teknolojia

Huawei wamesema hadi sasa programu endeshaji hiyo imeshapata makampuni 20 ya utengenezaji vifaa yaliyoonesha nia ya utumiaji wa HarmonyOS. Pia tayari kuna makampuni 280 ya utengenezaji apps ambayo tayari yameomba ushirikishwaji wa karibu katika utengenezaji wa programu endeshaji hiyo.

Programu endeshaji ya Harmony OS inatengenezwa ili iweze kufanya kazi katika vifaa vya aina mbalimbali

Huawei wamesema wanategemea watumiaji wa simu za Huawei za kisasa kama vile mate X2 waweze kusasisha na kupata HarmonyOS kwenye simu zao kufikia mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu.

SOMA PIA  Sikiliza Habari za Kiswahili kwenye Simu yako ya Android Muda Wowote

Wengi bado wanaona inaweza ikawa vigumu bado kwa Huawei kufanya vizuri kwenye soko la kimataifa la simu janja, kwani bado ukosekano wa apps mbalimbali muhimu kama vile za familia ya Google kutaweza kuwa kikwazo kwa wengi.

Chanzo:CNTech
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania