Kumekuwako na ongezeko la mahitaji ya mitambo maalumu ya kuzuia wezi ya CCTV siku za hivi karibuni kutokana na ukweli kwamba kumekuwa na ongezeko la watu wasio waaminifu katika jamii. Teknokona inakulete makala hii ili kukupa uelewa juu ya mitambo hii, ili uweze kuielewa.
CCTV ni mfumo ambao unajumuisha kamera ambazo zinauwezo wa kurekodi video pamoja na kifaa kinachoweza kuhifadhi video ambazo zimerekodiwa na kamera hizo ambacho kinaitwa DVR ama NVR.
Zipo kamera za aina mbalimbali na maranyingi huchambuliwa kutokana na maumbo yake ama matumizi yake, katika uchambuzi wa maumbo zipo kamera za bullet ambazo zinaumbo kama la risasi na ambazo mara nyingi hufungwa madhingira ya nje. Aina nyingne kutokana na umbo ni kamera za dome ambazo hizi huwa na umbo la dome ambalo ni la mviringo kamera hizi mara nyingi hutumika katika maeneo ya ndani ya nyumba.
Wakati mwingine kamera huchambuliwa kufuata matumizi yake katika kipengele hiki maanayake utapata kamera za aina mbili zile za kawaida na za kuzunguka ambazo huitwa PAN TILT ZOOM ama kwa kifupi PTZ. Kamera za kawaida ni zile ambazo ukiifunga basi huangalia eneo moja tu ambalo umeielekezea kwa wakati huo tuu wakati zile za PTZ zenyewe zinaweza kuzunguka pande tofauti na zinakuwa controlled kwa kutumia umeme.
Uchambuzi huu wa aina ya kamera bado haukutoshi wewe kuweza kwenda kununua kamera dukani maana bado itabidi ujue ni teknolojia gani ya kamera unataka kutumia, zipo teknolojia mbili kuu katika teknolojia ya kamera.
Kamera zinazotumia mfumo wa Analojia.
Kamera hizi hutumia waya mmoja wa ambao unabeba signal za data kutoka katika kamera hadi katika chombo cha kurekodia. Ingawa kamera hizi hazina garama kubwa ukiringanisha na teknolojia nyingine lakini zinakuja na gharama kwa sababu ni lazima ufanye mpango wa kuzipa umeme na hii inaweza kuongeza gharama.
Hii ni teknolojia ya zamani kidogo lakini bado inaweza kutumiaka hadi sasa kwa maana ni ya gharama za chini hasa kwa matumizi ya nyumbani.
Kamera zinazotumia mfumo wa IP.
Teknolojia ya IP ni teknolojia mpya ukilinganisha na teknolojia ya analojia, teknolojia hii inatumia waya za network kwa ajiri ya kusafirisha data ila katika nyakati nyingine zinaweza kutumika kusafirisha hata umeme wa kamera pia. Teknolojia hii ni ghari ukilinganisha na teknolojia ya analojia lakini inafaida nyingi zaidi (nitaandika makala nyingine juu ya faida na hasara za teknolojia hizi mbili.)