Ni kazi nyepesi kutumia programu moja, kwa mfano Google Playstore kusasisha programu zako zote kwa wakati mmoja. Mfumo huu wa kusasisha app au programu za simu na kompyuta sehemu moja umeonekana kupendelewa na watu wengi duniani na kupelekea mifumo-endeshaji ya Mac, iOS na Linux kujipatia sifa zaidi ya mifumo ya ‘Desktop’ ya Windows.
Je, unajua kwamba kuna programu kadhaa zinazoweza kusaidia kutatua adha hii kwenye kompyuta za Windows?
Angalia programu hizi za kusasisha(‘update’) programu za windows kirahisi kama ilivyokuwa kwenye mifumo mingine.
Ninite
Ninite ni rahisi sana kutumia na inapendwa na watu wengi kwa sababu hiyo. Programu hii uwezo wa kusasisha programu nyingi na pia unaweza kutumia Ninite kwenye kompyuta mpya, isiyokuwa na programu yoyote, ili kujirahisishia maisha. Utaweza kuchagua programu nyingi muhimu na kuziacha zikipakia kwenye kompyuta yako huku ukiendelea na mambo mengine ya msingi. Programu hizo ni zikiwemo vicheza muziki maarufu kama AIMP player, vivinjari vya Google Chrome na Mozilla, Skype na Viber. Pia, ukilipia Ninite, utaweza kushughulikia kompyuta zaidi ya moja kwenye mtandao. Hii ni muhimu kama unataka kumudu kompyuta za kampuni au ndugu zako.
Unaweza kuipata Ninite kupitia ->> Hapa
Download App
Download App inatoka cnet download.com, moja ya tovuti maarufu na ya kuaminika kwa kushusha programu za mifumo mbalimbali, ikiwemo windows.
Kazi ambayao Download App inafanya ni kutafuta programu kwenye kompyuta yako na kukutaarifu kuingia kwenye tovuti ya download.com na kushusha programu iwapo zimepitwa na wakati. Pia, kama ziada, programu hii inasafisha kompyuta yako iwapo ikidaka programu chakavu na data zingine zisizohitajika kwenye kompyuta yako.
Unaweza kuipata Download App kupitia ->> hapa.
Patch My PC
Patch my PC inafanya kazi kama Ninite. Tumia Patch my PC kushusha na kusasisha programu nyingi muhimu kwenye kompyuta yako. Unapoiweka kwenye kompyuta yako, Patch My PC inatafuta programu zote ulizonazo na kuzisaisha. Patch itapakia programu mpya na kukuchagulia mipangilio (settings) za kawaida. Patch My PC haitaweka programu za ziada, ambazo hujachagua.
Unaweza kuipata Patch My PC kupitia tovuti ya ->> hapa
No Comment! Be the first one.