Faini ya dola 50 au siku 15 jela – sheria moja imependekezwa katika jimbo moja nchini Marekani ambayo kama itapita itafanya utumiaji wa simu au tableti kwa utumaji wa meseji, mziki n.k wakati mtu anatembea kuwa kosa.
Maeneo ambayo sheria hiyo itabana ni pamoja na maeneo ya barabara – data za nchini Marekani zinaonesha kuna ongezeko kubwa la ajali zinazosababishwa na watembea kwa miguu wanaokuwa wamejikita sana katika utumiaji wa vifaa kama simu wakati wanatembea.
Kosa hilo lililopendekezwa kwa kutumia jina la ‘distracted walking’ tayari lipo katika sheria zinazosuburia kupitishwa kwenye jimbo jingine pia nchini Marekani – la Hawaii, ambapo wao wameweka faini ya hadi dola 250 kama mtu atapatikana na kosa la kuvuka barabara huku akiwa anatumia simu.

Data kutoka bodi ya usalama nchini Marekani inaonesha kulikuwa na kesi za majeruhi 11,101 kati ya mwaka 2000 hadi 2011 zilizosababishwa na utumiaji simu. Huku majeruhi wengi wakiwa wanawake, huku wengi wao wakiwa na umri wa miaka 40 na chini ya hapo.
Mapendekezo ya sheria kama hii yashashindwa kufanikiwa katika majimbo mengine kama vile Arkansas, Illinois, Nevada na New York.
Je una maoni gani juu ya sheria kama hii dhidi ya kutembea huku unatumia simu? Inaweza saidia au si ya ulazima?
Chanzo: theGuardian na mitandao mbalimbali