Jokofu ni moja ya vifaa ambavyo ni muhimu katika nyumba, ingawa watu familia nyingi zinamiliki majokofu lakini ni watu wachache sana ambao wanajua na kufata hatua stahiki kutunza majokofu yao.
Kutambua changamoto hii katika jamii Teknokona inakuletea vidokezo vya kuweza kukusaidia kuelewa kifaa chako.
-
Usafi wa koili husaidia kuhakikisha kifaa kinafanya kazi kwa ufanisi
Walau mara mbili kwa mwaka safisha coil zile zinazokuwa nyuma kwa kutumia brush laini, hii ni sehemu muhimu ya ufanyaji kazi wa kifaa hiki muhimu pindi coil hizo zinapokuwa na uchafu kama vumbi na mengineyo kunazuia kasi ya kubadilishana joto kati ya kifaa hiki na hewa inayozungusha.
2. Umbali kutoka ukutani unaweza kuwa ni chanzo cha kukosekana hewa ya kusaidia upoozaji
Nyakati zote hakikisha kwamba jokofu lako lipo umbali wa kutosha kutoka kitu chochote ambacho kitazuia kwa namna yeyote ile mzunguko wa hewa wa kutosha ili kusaidia ufanyaji wa kazi wa jokofu.
3. Mipira ya milango inahusika saana katika kuhakisha kwamba hakuna hewa inatoka ndani ya kifaa na kupunguza ubaridi.
Mara kwa mara unaposafisha Jokofu lako hakikisha kwamba unasafisha milango na mipira ya kwenye mlango wa kifaa hiki kwa kuwa mara nyingi huwa inaweka uchafu ambao husababisha jokofu lishindwe kutunza ubaridi, pindi unapogundua kwamba mipira ya kwenye mlango imechakaa hakikisha inabadilishwa.
4. Kuyeyesha kila kitu walau mara mbili kwa mwaka kutasaidia kuongeza ufanisi wa kifaa chako.
Walau mara mbili kwa mwaka hakikisha unayeyusha kila kitu, mara nyingi majokofu yetu huwa yanagandiana kutokana na kuwa yamekuwa yakifanya kazi kwa muda mrefu. Kuyeyesha walau mara mbili kwa mwaka kutapunguza kiasi cha nguvu kinatumika kugandisha barafu isiyo kuwa na faida kwa mtumiaji
Japo vipo vitu vingi unatakiwa kuvijua kuhusu majokofu lakini hivyo tulivyo vitaja hapo juu ni vile ambavyo vinaweza kufanyika katika jokofu lolote, kujua kuhusu jokofu lako unatakiwa kusoma maelezo ya kulitumia ambayo mara nyingi huwa yanakuja na kifaa unapo nunua.