fbpx

Facebook Pages: Kuonekana/kutoonekana kwa ukurasa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Moja ya mbinu ambayo viongozi wa ukurasa/kurasa kwenye Facebook sidhani kama wengi wetu tunafahamu ni kuwa unaweza kufanya kurasa kutoonekana.

Kutengeneza au kufuta ukurasa kwenye Facebook ni vitu ambavyo wengi wetu tunafahamu lakini kuhusu kuwezezekana kuficha ukurasa usionekane kwa wengine kama wapo tunaofahamu basi ni idadi ndogo sana.

Lazima tuelewe kuwa zipo sababu mbalimbali ambazo zinaweza zikasababisha kiongozi wa kundi akaamua kuwa ukurasa husika usionekane tena machoni pa watu mathalani kufanyiwa marekebisho ambayo wahusika hawataki wengine wayaone mpaka pale yatakapomalizika lakini wale wote ambao wana vyeo kwenye kurasa hizo wataweza kuona kama kawaida.

Sasa kitu cha kwanza kujua ni kwamba viongozi wa kurasa husika (admin) ndio ambao wanakuwa na uwezo wa kufanya ukurasa uonekane/kutoonekana na sio mtu mwingine yeyote.

Hivyo unaingia kwenye ukurasa husika kisha bofya Settings>>General>>Page-Visibility>>Page unpunished/published.

kutoonekana

Hatua za kufuata ili kuweza kufanya kurasa kwenye Facebook kuonekana/kutoonekana.

Kwa kuhitimisha nasema ni lazima ujue kuwa iwapo umetafuta ukurasa ambao ulikuwa upo siku za nyuma lakini kwa sasa haonekani tena basi ujue aidha umefutwa au umefichwa ili wengine wasiuone isipokuwa tu viongozi wa huo ukurasa.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Mwanzilishi wa WhatsApp awasihi watu wafute akaunti Facebook
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.