fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Google Maujanja Teknolojia

Jinsi ya kusajili Biashara yako Google Business

Jinsi ya kusajili Biashara yako Google Business

Spread the love

Katika ulimwengu wa sasa ni vyema mtu kufikiria kuiingiza biashara yako mtandaoni ili uweze kuongeza uwezekano wa kupata wateja wapya wa kuwahudumia na pia kujipa nafasi ya kuperuzi na kufahamu njia mbalimbali unazoweza kutumia kukuza biashara yako kupitia mtandao.

Tunaposema kusajili biashara yako Google usiogope ukidhania ya kwamba utatakiwa kuwa na tovuti hapana unaweza usiwe na tovuti lakini bado ukasajili biashara yako mtandaoni.

Google ni kampuni kubwa ya kiteknolojia iliyojikita katika kutoa huduma mbalimbali mtandaoni ikiwemo kutuma ujumbe wa kielektroniki na kupakua app mbalimbali Play store. Lakini pia unaweza ukaitumia Google kusajili biasahara yako mtandaoni ambapo mtu anayefahamu jina la duka lako au anayefahamu aina ya huduma unazotoa anaweza akakutafuta Google na kukupata. Mfano mtu anajua una duka la dawa mbezi basi anaweza akatafuta google maduka ya dawa yaliyopo mbezi na akaletewa orodha ya maduka ya dawa yaliyopo eneo hilo mojawapo litakuwa lako.

Hatua za kufuata unapotaka kusajili biashara yako Google:

  1. Hatua ya kwanza ni kutengeneza akaunti ya Google lakini kama tayari unayo unaweza ukairuka hatua hii. Ukiwa unatengeneza akaunti mpya utatakiwa kujaza jina lako la kwanza na la mwisho pamoja na nywila yako.kusajili Biashara yako Google
  2. Hatua inayofuata utajaza namba yako ya simu, terehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa pamoja na jinsia yako. Baada ya hapo akaunti yako ya Google itakuwa tayari na utaweza kuingia sasa katika upande wa kusajili biashara yako Google.
  3. Tembelea https://www.google.com/business/ kisha jaza taarifa za Biashara yako kama jina la biashara yako na aina ya biashara unayofanya.kusajili Biashara yako Google
  4. Jaza eneo ambalo Biashara yako inapatikana ukianza na nchi, mkoa au mji na mtaa. 
  5. Unaweza pia kujaza maeneo ambayo utaweza kumpelekea mteja wako bidhaa yake aliyonunua kwako. Utajaza pia na namba zako za simu pamoja na tovuti yako (Kama unayo).
  6. Utatakiwa kufanya uhakiki wa Biashara yako ambapo Google watakutumia barua yenye kadi ndani yake ambayo itakuwa na PIN namba za wewe kujaza ili kuihakiki hiyo biashara yako kama mmiliki halisi wa biashara hiyo. Hatua hii huwa inachukua takriban wiki mbili ila haikuzuii kuendelea na hatua zinazofuata.kusajili Biashara yako Google
  7. Weka masaa ambayo utakuwepo kazini pamoja na siku zako za kazi.
  8. Ruhusu kupokea ujumbe.
  9. Andika maelezo mafupi kuhusu biashara yako pamoja na Huduma unazozitoa.
  10. Weka picha za bidhaa zako pamoja na biashara yako.

Ni matumaini yangu kuwa umesoma na kufuata hatua hizo za kuisajili biashara yako Google endelea kufuatilia tovuti yetu kupata msaada zaidi na ushauri wa kibiashara. Pia unaweza kusoma makala zetu zingine hapa.

SOMA PIA  Unaona Simu nyingi zimeanza kufanana sana? Makampuni mengi wanatengeneza kwa makandarasi

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania