Imekuwa kama desturi ya makampuni mengi kutoa simu janja ambazo zinakuwa zina jina moja huku zitofautiana aidha kwa namba au kwa vivumishi fulani fulani. Samsung mi moja ya makampuni hayo ambapo wapo mbioni kutoa Galaxy F13.
Imeonekana kuwa wakati umewadia kwa Galaxy F12 kuwa na ndugu yake kwenye soko la ushindani. Hii imebainika mara baada ya kuonekana sifa za Samsung Galaxy F13 kwenye tovuti ya Geekbench huku simu hiyo ikitambulika kwa namba maalum (SM-E135F). Kimsingi simu hii itakuwa ikifanana kwa karibu sana na Samsung Galaxy A13 kwa sababu mbalimbali, zikiwemo:-
- urefu wa kioo kuwa inchi 6.6 aina ya LCD lakini kuwa na ung’avu wa hali ya juu (FHD+),
- kamera kuu ya 50MP na
- betri yenye mAh 5000.
Kwa upande mwingine simu hii inafanana na mtangulizi wake kwenye maeneo kadhaa kama vile kipuri mama (Exynos 850) lakini pia RAM ya 4GB kama ilivyo kwenye Samsung Galaxy F12.
Kuhusu ujio wa simu hii bado haujafahamika wazi lakini pengine ikatoka mwaka huu ndani ya miezi michache ijayo watu wakaweza kufahamu/kununua simu hiyo. TeknoKona tutazidi kukubaharisha kuhusiana na habari hii pamoja na nyingine nyingi tuu.
Usisahau kuwa hivi sasa tuna programu tumishi yetu-Tech Msaada ambayo imeshseni vitu vingi halikadhalika uwezo wa kusoma makala zetu zote ambazo zipo kwenye tovuti. Ipakue kutoka kwenye Playstore kuweza kufahamu mengi.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.