fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps instagram Teknolojia

Uwezo wa kuficha idadi ya watu waliopenda kitu kwenye Instagram

Uwezo wa kuficha idadi ya watu waliopenda kitu kwenye Instagram

Programu tumishi-Instagram kwa mara nyingine tena inaongezewa kipengele kinachoficha idadi ya watu waliotokea kupenda chapisho aliloliweka.

Nianze kwa swali rahisi tuu, ni mara ngapi kwa siku unaperuzi kwenye Instagram? Ukiwa unafikiria jibu fahamu kwamba Facebook wanajaribu kwa mara nyingine tena kipengele cha kuficha idadi ya watu waliopenda chapisho lake kwenye Instagram. Mwaka 2019, kipengele hicho kilionekana kwa mara ya kwanza na mrejesho wake ukawa hasi na chanya; kuna wengine walionena ni kitu kizuri kwa maana ya usiri wa aina fulani huku wengine (hasa watu maarufu) wakiona si kizuri kwani wanapenda kufuatilia machapisho ambayo yametokea kuvutia watu wengi zaidi.

SOMA PIA  eSIM: Teknolojia ambayo haijaenea sana

Hivi karibuni kwa mara nyingine tena Facebook wameona wakilete tena kipengele hicho kwenye Instagram ambapo huenda kikadumu ama la! Zipo taarifa kuwa kipengele hicho pia kinaweza kikaenda mpaka kwenye Facebook kwani tukumbuke kuwa zote hizo zinatoka kwenye familia moja.

Hivi sasa Facebook imeweka kipengele hicho kwenye hatua ya jaribio kwa baadhi ya watu kuweza kuamua iwapo wanapendezwa kuona watu walipoenda na idadi yao kwa ujumla wake ama waone fulani kapenda hiki bila ya kupata namba kamili.

kuficha idadi

Kipengele cha kuficha idadi ya watu kwenye Instagram chaingia kwenye majaribio tena.

Nchi ambazo kipengele hicho kimeruhusiwa kuonekana ni Canada, Australia, Brazil, Ireland, Italia, Japan,  New Zealand pamoja na baadhi ya watu waliojumuishwa kwenye kundi la kukifanyia majaribio kipengele hicho kisha kutoa mrejesho kama ni kizuri au kibaya. Iwapo mtu amewekwa kwenye kundi la majaribio ataonamaelezo yalijitosheleza kumtaarifu kuwa anaweza kuona tofauti.

kuficha idadi

Kwa yeyote ambaeamewezeshwa kujaribu kipengele cha kuficha idadi ya watu walioenda chapisho atauona huo ujunbe hapo juu.

Tuambie ewe msomaji wetu ni mioni mwa wale walio na uwezo wa kujaribu kipengele hicho? Unakizungumziaje bila kujali kama umewezesha kukijaribu au la! Tunakaribisha maoni yako.

Vyanzo: E-Commerce News, Gadgets 360

SOMA PIA  Helios Towers, wamiliki na waendeshaji minara Afrika sasa kwenye soko la hisa Uingereza.
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania