fbpx
Tanzania, Teknolojia

BRELA: Usajili wa Kampuni na Biashara sasa kwa Mtandao

brela-usajili-wa-kampuni-na-biashara-sasa-kwa-mtandao
Sambaza

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) unatarajia kuzindua mfumo wa usajili wa kampuni na biashara kwa njia ya mtandao.

brela

Baada ya mchakato wa muda mrefu, mfumo huo utazinduliwa mwezi ujao lakini kila Mtanzania anapaswa kuwa na kitambulisho kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) ili kuhudumiwa kwa urahisi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Frank Kanyusi amesema wageni kutoka nje ya nchi wanatakiwa kutumia namba za pasi zao za kusafiria.

INAYOHUSIANA  Walemavu wa kusikia na matumizi ya simu Tanzania
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Frank Kanyusi

“Huduma hii imekamilika tangu Juni 2 na itazinduliwa rasmi Agosti mwaka huu. Kitambulisho cha taifa ni muhimu kwa sababu ni hitaji la kwanza kufanikisha usajili,” alisema Kanyusi.

Awali, huduma ya mtandao ilikuwa ni kwa ajili ya majina ya biashara lakini sasa imepanuliwa na kuruhusu usajili wa majina ya kampuni.

Licha ya Nida, Brela sasa inashirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenye huduma zake.

INAYOHUSIANA  Teknolojia ya magari ya umeme yaingia Serengeti

Baada ya mhusika kutembelea tovuti ya Brela na kuingiza namba ya kitambulisho chake cha taifa au pasi ya kusafiria, Kanyusi alisema taarifa hizo zitapelekwa TRA ambao watatoa namba za utambulisho wa mlipa kodi itakayokuwa pia na cheti cha kampuni.

“Tumeamua kufanya hivi ili kupunguza mizunguko kwa sababu zamani mtu akitaka kusajili jina la kampuni au huduma nyingine kutoka BRELA alitakiwa kuzunguka ofisi nyingi kupata uhakiki wa taarifa zake, lakini sasa taarifa zote zinapatikana kwa wakati mmoja,” alisema.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.