fbpx
Google, Mtandao wa Kijamii, Teknolojia, TikTok

Inaaminika kuwa TIkTok ilikusanya taarifa za watu bila idhini yao

inaaminika-kuwa-tiktok-ilikusanya-taarifa-za-watu-bila-idhini-yao
Sambaza

Moja ya programu tumishi ambayo imetokea kupendwa sehemu nyingi duniani katika kipindi cha muda mfupi ni TikTok na katika siku za karibuni kampuni mama imejikuta katika hali ngumu kutokana na kashfa mbalimbali dhidi yao.

Kama ni wakati mgumu basi TikTok inapitia mengi hivi sasa na tayari tumeshasikia kuhusu amri ya kufungwa kutumika huko nchini Marekani lakini pia Instagram kuleta “Reels” na kuonekana kama mpinzani. Kama hiyo haitoshi hivi karibuni imebadika taarifa kuwa katika kipindi cha angalau miezi kumi na mitano (15) TikTok ilikusanya taarifa za watumiaji wake na kuzituma kwenye kampuni mama, ByteDance.

Inaelezwa kuwa katika kipindi hicho TikTok iliwazunguka Google  kwa maana ya kwamba watumiaji wa Android hivyo wakawa wanachukuwa taarifa za kitambulisho cha kifaa (Mac address), utambulisho wa akaunti ya mhusika (advertising ID) na kisha kuzipeleka ByteDance kisha kuwapa makampuni yanayotangaza biashara wakatengeneza tangazo kulingana na kile ambacho mhusika anapenda kufanya kwenye TikTok kisha mtumiaji kuendelea kuona tangazo mpaka plae atakapoacha kutumia programu tumishi husika.

INAYOHUSIANA  Bunge kuendesha shughuli zake kimtandao
taarifa za watu
Inaaminika hadi Novemba 2019, TikTok ilitumia njia ambayo Google ilishakataza kukusanya taarifa za watu wanaotumia Android.

Fahamu ya kuwa kwenye vifaa vyetu vya kidijitali kuna kitambulisho ambacho hakibadili, hakifanani na kingine. Kitu hicho kinaitwa Mac address.

Kitendo ambacho inaaminika TikTok walikifanya kwa mujibu wa taarifa iliyotoka hivi karibuni inakiuka kanuni za Google ilizoziweka kwa waundaji wote wa programu tumishi kuhusu ukusanyaji wa taarifa za watu.

Vyanzo: Android Police, Business Insider

Facebook Comments

Sambaza
2 Comments
Share
Tags: , ,

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

2 Comments

  1. TikTok kufungiwa Marekani: Muda umesogezwa mpaka siku 90
    August 17, 2020 at 2:47 pm

    […] ya mafanikio makubwa ya haraka, TikTok wapo kwenye hatihati ya kufungiwa nchini Marekani. Je, sababu ni nini? Fahamu […]

  2. TikTok kufungiwa Marekani: Muda umesogezwa mpaka siku 90 – ZANZICT
    August 24, 2020 at 4:56 am

    […] ya mafanikio makubwa ya haraka, TikTok wapo kwenye hatihati ya kufungiwa nchini Marekani. Je, sababu ni nini? Fahamu […]