fbpx

Android, apps, instagram, iOS, Mtandao wa Kijamii

Maboresho: Kuhusu kuficha maoni kwenye Instagram

kuhusu-kuficha-maoni-kwenye-instagram

Sambaza

Kuna mengi ambayo yanachapushwa kwenye mitandao ya kijamii ambayo yanaweza kuwa hasi au chanya kulingana na maudhui, jinsi kilivyopokelewa; kusababisha fedheha ama furaha na pengine hata kufikiria kuficha maoni.

Mara kwa mara Instagram imekuwa ikifanyiwa maboresho kulingana na maoni ambayo inapokea kutoka kwa wadau, makosa mbalimbali au jinsi ambavyo inaonekana inapendeza kulingana na mwenendo wa teknolojia kwa wakati huo. Katika kuadhimisha miaka kumi (10) tangu kuzinduliwa kwake, Oktoba 6 2010 programu tumishi husika imeboresha mambo ili kuendelea kuvutia watumiaji wake:

SOMA PIA  Hakiki App; Pata ripoti za Matumizi ya Pesa za Huduma za Kibenki za Simu (Mobile Money)

>Mosi, kuficha maoni yanaonekana ni ya kukera. Katika masasisho yaliyowekwa ni maoni yote ambayo yanaonekana yanakera yatafichwa bila ya hata wengine kuweza kuyoaona; jambo hili linafanyika lenyewe tuu (automatically). Hata hivyo, yule aliyeyachapisha kitu kwenye akaunti yake ana uwezo wa kuona maoni yote ambayo yamefichwa.

kuficha maoni
Instagram inatumia teknolojia ya juu kuweza kuelewa ujumbe ulioandikwa kama ni wa kukera au vinginevyo ili kuweza kuficha maoni kwenye chapisho husika.

>Pili, uwezo wa kutangaza biashara kupitia IGTV. Kwa wale ambao tunatumia Instaram kama sehemu ya kutangaza biashara zetu ninaamini kuwa tunafahamu kuhusu kipengele cha IGTV ndani ya programu tumishi husika. Katika maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Instagram, programu tumishi husika imewesha mtu kuweka bei ya vitu kulingana na chapisho lililowekwa kwenye kipengele cha IGTV. Kipengele hikihiki kitaonekana kwenye Reels baadae mwaka huu.

SOMA PIA  Skype Kutengenezwa Upya Kuwa Kama Snapchat Kwa Microsoft!
kuficha maoni
Hivi sasa mtu anaweza akaweka chapisho kwenye IGTV na kisha kuweka bei ya kile ambacho anakiuza.

Hao ndio Facebook ambao wanaendelea kuhakikisha programu tumishi inazozimiliki zinaondoloea karaha watumiaji wake hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuendelea kuvutia. Kitu cha kufanya ni kupakwa masasisho hayo mapya ili kuweza kufurahia mabadiliko husika.

Vyanzo: TechCrunch, Gadgets 360.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

    Toa Maoni

    Your email address will not be published. Required fields are marked*