fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps Google Teknolojia

Google Podcast na downloads milioni 100, App ya Podcast ya Google yapaa kwa watumiaji

Google Podcast na downloads milioni 100, App ya Podcast ya Google yapaa kwa watumiaji

App ya Google Podcast na downloads 100 kwenye Android. App hiyo imeshushwa (download) mara milioni 100 na hivyo kuwa app maarufu zaidi kwa ajili ya kusikiliza vipindi vya Podcast katika simu za Android.

Je, Podcast ni nini?

Podcast ni mfumo wa usambazaji wa vipindi katika mfumo wa sauti. Kupitia huduma za Podcast utaweza kusikiliza vipindi mbalimbali kwa urahisi na kwa muda utakao wewe kupitia simu yako. Fahamu zaidi kwa kusoma makala yetu hapa – Podcast ni nini?

Google Podcast na downloads milioni 100

Google Podcast na downloads milioni 100. App hii inapatikana kwa watumiaji wa Android pamoja na wa iPhone (iOS)

Google wameleta app yao kwa ajili ya usikilizaji wa vipindi vya Podcast mwaka 2018, tofauti na apps nyingi za Google ambazo huwa zinakuja moja kwa moja pamoja na simu za Android hali ni tofauti kwa app ya Google Podcast. Hii inapatikana kwa kupakuliwa kutoka kwenye soko la apps.

SOMA PIA  Miundombinu ya TEHAMA na intaneti nchini Tanzania #Uchambuzi #Ripoti

Ukuaji wa kufikisha milioni 100 umekuwa wa kasi sana kwani ni miezi mitano tuu tokea app hiyo ifikishe downloads milioni 50, hivyo inaonekana imepata umaarufu wa haraka sana hivi karibuni. App ya Podcast ya Google imerahisishwa kuhakikisha unaweza kufuatilia vipindi utakavyo na pia utaweza kushauriwa vipindi vingine kwa urahisi pia.

Kupakua app ya Google Podcast tembelea Google Playstore kwa Android, na kwa watumiaji wa iPhone tembelea Apple AppStore.

Vyanzo: AndroidPolice na vyanzo mbalimbali
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania