fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung Teknolojia

Samsung yashinda jumla ya tuzo 71

Samsung yashinda jumla ya tuzo 71

Kitu chocohote kile kizuri unachokifanya halafu ikatokea ukapongezwa kwa namna yoyote ile hakika inaletaa furaha na hamaasa ya kuendelea kufanya vizuri zaidi ndivyo hivyo Samsung wamefanikiwa kunyakua jumla ya tuzo 71 za iF Design Awards mwaka 2021.

Samsung Electronics ambayo hakuna asiyeijua duniasni kote hivi karibuni imewafikiwa kuwafurahisaha jopo la majaji mara 71 kwenye tuzo za “iF Design Awards“. Tuzo hizi za iF Design Awards ni mahususi kwa ajili ya kutathimini muundo vitu mbalimbali vya kidijiti kwenye vipengele mbalimbali kama utalaamu wa uundaji, ufungaji, urahisi wa kutumia kitu, muundo wa ndani kwenye kitu husika, n.k. Tuzo hizo zimekuwa zikifanyika tangu mwaka 1953.

SOMA PIA  BlackBerry Messenger (BBM) kufungwa Mei 31

SAmdung ambao wameshinda jumla ya tuzo 71; 36 kati ya hizo zimetokana na bidhaa zao, 10 kwenye kipengele cha “Professional concept“, 11 kutoka kapu la “Communication designs“, 5 zikihusu “Packaging design” na 9 kutokana na kuvutia “User experience and interface“.

Karibu vitu elfu kumi vilitumwa na kampuni mbalimbali kutoka nchi 52 kuweza kutafuta nafasi ya kushinda tuzo za iF Design Awards mwaka 2021.

Bidhaa mbalimbali za Samsung zilizowezesha kushinda tuzo

Simu janja Samsung Galaxy Z Fold 2 na Z Flip ni miongoni mwa bidhaa zilishinda tuzo pamoja na runinga ya kisasa aina ya QLED 8K kutokana na muundo wa aina yake lakini pia ubora wa muonekano wa picha ndani runinga hizo.

tuzo 71

Simu janja za Samsung Galaxy Z Flip na Z Fold 2.

tuzo 71

Runinga janja ya Samsung QLED 8K.

Mbali na hilo  bidhaa ya Samsung mahususi kwa ajili ya kuonyesha vitu kwenye ukuta, kitambaa/ubao mweupe, n.k kwa Kiswahili kirahisi tunasema projekta ni bidhaa nyingine iliyopeleka tuzo kwa Samsung Electronics baada ya kuwavutia majaji kutokana na muundo wake.

tuzo 71

Projekta ya Samsung iliyofanya Samsung washinde tuzo za iF Design Awards 2021.

Ushindi huu ni mkubwa na kuweka alama ya aina yake lakini pengine kuwafanya waendelee kutoa vitu vizuri na vya ushindani kweli kweli. Vipi unazungumziaje habari hii? Tunakaribisha maoni yako.

Vyanzo: GSMArena, Tovuti ya iF Design Awards

SOMA PIA  Apple yapata pigo baada ya taarifa kuhusu bidhaa zake kuvuja
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

  1. […] post Samsung yashinda jumla ya tuzo 71 appeared first on TeknoKona Teknolojia […]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania