Teknolojia mpya ya utengenezaji betri iliyotengenezwa na mwalimu na mwanafunzi wake wa PhD huko nchini Korea Kusini itawezesha kifaa kama simu kukaa na chaji kwa wiki moja nzima bila kuchaji.
Profesa Choi na mwanafunzi wake wa chuo kikuu cha Pohang wametengeneza betri la aina ya ‘solid oxide’ {solid oxide fuel cell (SOFC)} wakiwa na lengo la betri hilo kutumika badala ya betri za sasa hivi ambazo ni za ‘lithium-ion’.
Betri zinazotumika katika simu, tableti, drone na vifaa mbalimbali vya elektroniki kwa sasa ni za teknolojia ya Lithium-ion. Betri hizi zinakiwango kidogo za uhifadhi wa chaji.
Teknolojia hii iliyogunduliwa na Profesa Choi na mwanafunzi wake, Bwana Kun Joong Kim imepokelewa vizuri kwani inaweza kutumika ata kwa betri kubwa kama zile zinazoitajika kwenye magari yanayotumia umeme. Teknolojia inayokua kwa kasi kwa sasa.
Teknolojia hii inategemea utumiaji wa Hydrogen, ikiwa pia na sifa ya utengenezaji usio mgumu sana huku ‘electrolyte’ zake zikiwa na sifa kubwa ya kutopotea kwa urahisi – hivyo uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu.
Kwa teknolojia hii vifaa kama simu janja zitaweza kuchajiwa mara moja tuu kwa wiki huku vifaa kama vile drones vitaweza kutumika kwa zaidi ya lisaa limoja. Hii ni tofauti na sasa ambapo simu nyingi huchajiwa kila siku huku drone zikiweza kurushwa chini ya lisaa limoja kabla ya kuitaji kuchajiwa.
Je una maoni gani juu ya teknolojia hii? Uwezo wa kuchaji simu mara moja tuu kwa wiki utakuwa muhimu sana?
Chanzo: postech.ac.kr