Kuna vitu usipokuwa mtu wa kupita huku na kule inakuwa ni nguvu kujua kama vimetoka. Xiaomi Redmi Note 6 Pro imetoka bila hata ya tovuti nyingi kunasa habari zake.
Simu hii ambayo nitaiangazia kwenye makala ya leo imezinduliwa na taarifa zake zimebainika kupitia tovuti rasmi kwa Thailand na mpaka sasa si watu wengi ambao wameweza kufahamu undani wa Xiaomi Redmi Note 6 Pro. undani wake ni kama ifuatavyo:-
Kipuri mama+Kioo.
Simu husika imewezeshwa kwa kuwa na Snapdragon 636 na kuhakikisha kuwa na kasi ya kuridhisha kutokana ni kipuri ambacho ni toleo ambalo halina miaka mingi tangu kutambulishwa. Kioo chake kina urefu wa inchi 6.26 aina ya IPS LCD na ikiwa na ulinzi wa kioo kigumu Gorilla 2.5D.
RAM+Diski uhifadhi.
Xiaomi Redmi Note 6 Pro imewekwa RAM ya ukubwa wa GB 4 ikiwa na memori ya ndani ambayo ukubwa wake ni GB 64.
Kamera+Betri.

Xiaomi kwa mara ya kanza wametoa simu yenye kamera nne kwa ujumla wake na ukitaka kujua kwa undani zaidi ni kwamba zile kamera za nyuma moja ina MP 12 na nyingine ni MP 5. Upande wa mbele zipo kamera mbili (ambapo ni kwa mara ya kwanza kabisa) zikiwa na MP 20+MP 2 mtawaliwa. Betri yake ina 4000mAh ikiwa na uwezo wa kutunza chaji kwa saa sita iwapo utaitumia kwa kucheza magemu au saa nane nane na nusu iwapo itatumika kuangalia picha jongefu.

Rangi+Bei pamoja na mengineyo.
Haijawekwa kwenye rangi kadha wa kadha isipokuwa tatu tu ambazo ni Bluu, Nyeusi na Dhahabu. Kwa hakika wengi wetu tutaweza kuinunua simu hiyo kutokana na bei yake kuwa ya kuridhisha, $215|Tsh. 494,500. Mambo mengineyo yanayoihusu simu hiyo ni kuwa na umbo la herufi “V”, inatumia kadi mbili za simu, Wi-Fi, GPS, Bluetooth, 3G, 4G, inatumia USB yenye upana mdogo.

Upatikanaji wa Xiaomi Redmi Note 6 Pro ni kwa kuagiza kutoka Thailand, kuhusu taarifa za kuanza kupatikana kwingineko duniani bado hazijafahamika.