Una wafanyakazi walio busy sana au ni wavivu tuu kurudishia viti vizuri baada ya kuvitumia? Basi viti vilivyo kwenye ofisi za kampuni ya magari ya Nissan ndio vinavyoitajika…. Viti vinavyojipanga vyenyewe!
Kama sehemu ya kuzipa promo gari zao mpya zenye teknolojia janja inayoziwezesha kuweza kujipaki zenyewe kampuni ya Nissan imeonesha viti vinavyotumika katika ofisi zake ambavyo ata pale mtumiaji akinyanyuka na kuondoka bila kurudishia ndani viti hivyo hujirudishia vyenyewe baada ya kupewa amri.
Viti hivi unaweza sema ni virobi vinavyopewa maelekezo na kamera janja zilizopo katika kuta zote zinazotazama viti. Nissan wametumia kuonesha teknolojia hii kama promo ya kutangaza magari yao mapya yenye uwezo wa kujipaki yenyewe.
Viti hivyo vilivyotengenezwa na kampuni ya viti ya Okamura ya huko nchini Japan vimefanyiwa maboresho machache ili kufanikisha uwezo huo. Upigaji wa makofi mara moja unafanya viti vyote kusogea na kujiweka katika eneo lake usika.
Nini kimetumika?
- Viti hivyo vimeunganishwa pamoja kutumia teknolojia ya wiFi, na kamera janja zenye ‘sensor’. Upigaji wa makofi utafanya viti vyote kujipanga vizuri mara moja.
- Ni kutumia kamera hizo zenye ‘sensor’ pamoja na teknolojia ya WiFi viti hivyo vitarudishwa kwenye eneo lake la awali. Kamera janja hizo zitafanya kazi kama macho ya binadamu kuangalia viti vimekaaje na kisha kupitia amri inayopelekwa kupitia WiFi basi viti hivyo vitajipaki kulingana na maelekezo yaliyotumwa kupitia taarifa zilizochukuliwa na kamera janja hizo.
Angalia GIF
Angalia video
No Comment! Be the first one.