Facebook imekuwa ikifanyia majaribio ya huduma za ujumbe mfupi (SMS) kwa baadhi ya watumiaji wa app ya Messenger ya Android, hatua hii ikifanikiwa itawaruhusu watumiaji wa Messenger kuweza kusoma na kujibu SMS zao kupitia app hiyo.
Huduma hizi mpya zinajaribiwa kwa baadhi ya watumiaji wa Android ambao wanatumia app ya Messenger, hii ni kwa sababu Facebook inawashabiki wengi zaidi wanaotumia Android.
Huduma hii haitakuwa mara ya kwanza kuja kwa watumiaji wa Messenger ilishawahi kuwepo miaka ya nyuma lakini iliondolewa mwaka 2013 baada ya app kufanyiwa mabadiliko makubwa wakati huo. Na ilisemwa kwamba imetolewa kutokana na ukweli kwamba haikupata mashiko kwa wakati huo.
Mabadiliko haya ya sasa sio tu kwamb yanakuja na uwezo wa SMS bali sasa tutaweza kutumia akaunti zaidi ya moja katika app hii. Hii ni habari nzuri kwa mamilioni ya watumiaji ambao bado wana share simu kwaajiri ya facebook, kumbuka kwamba kunaidadi kubwa kwa watumiaji wa facebook ambao ni watu wa kipato cha chini ambao kwa namna moja au nyingine hawawezi kumudu gharama za simu janja.
Msemaji wa Facebook amekariliwa akisema kwamba Hivi sasa, wanajaribu uwezo wa kufanya watumiaji kuleta mazungumzo yao yote sehemu moja.
Kuunganishwa huduma ya SMS kuna maanisha kwamba badala ya kutumia app maalumu iliyo katika simu yako kwaajiri ya kusoma ujumbe utaweza kusoma ujumbe kutoka katika app ya Messenger iwapo tu utaamua kuwa Messenger iwe ndiyo app yako mahususi kwaajiri ya kusomea ujumbe wako mfupi.
Facebook na mitandao mingine ya kijamii kama twitter na instagram inategemea matangazo kujiendesha na kwa maana hiyo basi jambo la msingi kwao ni kuwa na watumiaji wengi hivyo kila wakati utaona hii mitandao inafanya kila njia na kila linalowezekana kuteka watumiaji wengi zaidi. Kuunganisha huduma ya SMS katika app ya Messenger kutawafanya watumaji wengi kutumia app hiyo zaidi hivyo kufukia lengo kuu la watumiji wengi.
Facebook hawapo peke yao katika vita ya kuhakikisha kuwa wana watumiaji wengi, Twitter pia juzi waliingia mtatani na watumaji wao baada ya kutaka kubadilisha namna ambavyo mtandao huo ulikuwa unafanyakazi (na ambayo ndiyo namna watumiaji wengi wanaupenda).
One Comment