Kampuni ya Apple imehusishwa kuungana na wataalamu wa nishati ili kuleta chaja ambazo hazitumii nyaya moja kwa moja, maarufu kama ‘Wireless’.
Mpaka sasa hakuna uhakika juu ya taarifa hizi kwani ni fununu tuu, lakini pia kumbuka lisemwalo lipo, kama halipo basi …..? Fununu hizo ziliongeza kwa kusema kuwa kampuni hilo linajikita zaidi katika kutengeneza chaja hizo za kizazi kipya kabisa
Vifaa vya Apple (iDevices) vyote vinaweza vikawa na mfumo huu wa chaja. Apple pia inasema kuwa katika vifaa vyake vya Iphone na Ipad ni kwamba kampuni linategemea kuona kuwa vifaa hivyo vinachajiwa katika umbali mrefu bila waya ukilinganisha na njia ya sasa
Fununu zimesema kuwa kampuni hiyo ya Apple inafanya kazi kwa kushirikiana na wenzao waliko marekani na wale waliopo katika bara la Asia ili kuhakikisha teknolojia hii inakuja mwanzoni tuu mwa mwaka ujao (2017).
Taarifa hizi zisizo rasmi zinasema kuwa Apple wataungana na Energous ili kuhakikisha wanakamilisha zoezi hili kama inavyosemekana.
Pia mwanzoni kabisa mwa mwaka 2015 kampuni ya Energous ilisema kuwa inaweza ikaingia katika ushirika na kampuni moja wapo ambayo ipo katika tano bora katika makampuni makubwa kabisa ya vifaa vya kielektroniki. Walisema kampuni hiyo inaweza ikawa Apple, HP, Samsung, Hitachi au Microsoft.
Katika makampuni yote yaliyotajwa hapo juu kampuni la Apple ndilo ambalo lina asilimia nyingi kupita wenzake kuwa watakuwa pamoja na Energous katika kutengeneza kifaa hicho.
No Comment! Be the first one.