fbpx

iPhone X yadumu kwa wiki mbili chini ya mto

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Teknolojia ya simu janja kutoingia maji katika teknolojia ambayo imeonekana kutumia na makampuni nguli kama vile Apple, Samsung imeonekana kuwa na matokeo mazuri sana.

Makampuni mengi wamezifanya simu rununu ambazo zina uwezo wa kutoingia maji katika umbali wa mita kadhaa kwa muda wa mpaka dakika 30 lakini katika hali ambayo haikutegemewa iPhone X iliweza kudumu chini ya maji (kwenye mto) kwa wiki 2 bila ya hata ya kuwa na ule ufuniko wa juu unaozuia simu hiyo kuingia maji.

Ilikuaje?

Bw. Dallas (mwana maji), ambaye ana chaneli yake kwenye Youtube iitwayo Man + River aliweza kupata iPhone X pamoja na vitu kama miwani za Porsche, pete ya dhaahbu yenye thamani ya $10 elfu.

chini ya mto

iPhone X ambayo ilitoka mwaka jana ina uwezo wa kutoingia maji kwa umbali wa kina cha maji mpaka mita moja kwa muda wa dakika 30 lakini simu hiyo iliyookotwa ilidumu kwa taribani wiki 2 chini ya mto.

Mwana maji huyo aliamua kuikausha kwa kutumia vifaa vya kawaida kabisa; mashine ya kukaushia nywele, mafuta ya silica yaliyokuwa yamejazwa kwenye jagi. Baada ya siku 3, Bw. Dallas alijaribu kuichaji na ikawaka bila shida yoyote.

INAYOHUSIANA  Simu mbili za Samsung kupata Android 9 Pie Januari 2019

Bw. Dallas alimtafuta mwenye simu na kumrudishia pia alibainisha kuwa simu hiyo ilipotea wiki 2 kabla ya mwana maji huyo kuipata. Kumbuka dhamana ya kurudisha simu kwa Apple haikubaliki iwapo simu imeharibika kutokana na kuingia maji.

Vyanzo: Gadgets 360, The Sun

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.