fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple IPhone Teknolojia

Njia rahisi ya kufanya malipo kwa njia ya kidijiti kwenye iPhone

Njia rahisi ya kufanya malipo kwa njia ya kidijiti kwenye iPhone

Spread the love

Teknolojia imekuwa ikipanuka siku hadi siku na kwa wale tunaofahamu si ajabu mtu kutembea na pesa nyingi tuu ambazo hazionekani kwa macho lakini zimehifadhiwa kwa njia ya kidijiti na mhusika ana uwezo wa kufanya malipo (miamala) bila wasiwasi wowote.

Ilikuwa ni habari za chini chini tuu lakini sasa ni kweli kwamba Apple wameongeza njia rahisi ya kuwezesha watumiaji wa iPhone (kuanzia iPhone XS na kuendelea) kuweza malipo/miamala bila kugusana au kuwa na fedha taslimu. Teknolojia hii kwa Kiingereza inaitwa “Tap to pay“.

SOMA PIA  Vilivyotangazwa na Apple katika Tukio la April 2021. #iMac #AirTag #M1

Maboresho hayo ambayo Apple imeyapeleka kwenye simu za iPhone XS au juu zaidi yanahusisha simu janja mbili au mojawapo inaweza kuwa saa ya Apple na mtu akaweza kulipia kitu fulani ili kuweza kununua bidhaa husika. Kwa lugha rahisi ni kutokuwepo kugusanagusana ili kuweza kufanikisha muamala.

kufanya malipo

Njia rahisi na ya haraka kuweza kufanya malipo kwenye iPhone/saa za Apple.

Teknolojia hiyo ambayo bado ni mpya kwa watumiaji wa iPhone inakubali kufanya miamala kwenye Apple Pay na vilevile waundaji wanaiboresha kuweza kufanya malipo kwenye mifuko ya kuhifadhia sarafu za kidijitali ama kwenye programu tumishi ambazo ni za kulipia.

Stripe ni moja kati ya kampuni ambazo zimeshaanza kuweka mifumo ya watu kuweza kufanya miamala bila ya kugusana/kupokea fedha taslimu.

Awali huduma hii itafanya kazi nchini Marekani kwa kadi za malipo kama American Express, Discover, Mastercard na Visa. Kwa maduka ya Apple yaliyopo nchini Marekani yataanza kukubali mtindo wa miamala baadae mwaka huu.

Vyanzo: Engadget, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania