Dunia inakabiliana na janga la mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanasababishwa na sababu nyingi zikiwemo matumizi ya nishati inayozalisha hewa chafu, uwepo wa magari kwa wingi barabarani yanayotumia mafuta. Watalamu wa teknolojia nao hawapo mbali katika matumizi ya teknolojia kufanya kazi kwa ufanisi mathalani upandaji wa mbegu za miti kwa wingi ndani ya muda mfupi.
Zipo njia mbalimbali ambazo zinatumika katika kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanaendelea kutafuna ulimwengu kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, kuna teknolojia ambayo imebuniwa na kampuni AirSeed Technologies iliyolenga kurahisisha shughuli nzima ya upandaji wa miti kwa haraka ndani ya muda mfupi.
Historia fupi/hali halisi
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa wanasema dunia imebakiza miaka 10 tu kuweza kuzuia mabadiliko makubwa ya tabia ya nchi yanatakayoyumbisha ulimwengu na hili linawezekana kwa kuacha kutumia nishati ya mafuta, kupanda miti, kutumia mbinu nyinginezo ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Inakadiriwa zaidi ya Km za mraba 1.3 za miti zimekatwa tangu mwaka 1990, miti bilioni 15 hukatwa kwa mwaka, tani milioni 1.35 ya Carbon huondolewa/hupotea kila mwaka.
AirSeed Technologies nini?
Hii ni kampuni inayochipuka ya nchini Australia ambayo imejikita kutumia teknolojia ya ndege zisizo na rubani kuweza kupanda mbegu za miti ili kuokoa mazingira. Zaidi ya hekta 40m za misitu zimeharibiwa kutokana na majanga ya moto misituni nchini humo.
Kampuni hii inatengeneza ndege hizo ambazo zina uwezo wa kupanda mbegu za miti 40 elfu kwa siku moja kulinganisha na mbegu 800 anazoweza kupanda mtu ndani ya saa 24. Teknolojia hii ni ya haraka mara 25 zaidi kuliko ile ya kawaida na rahisi kwa 80% ya ile njia ya kawaida.

Hakika shukrani kwa ukuaji wa teknolojia na kwa mwenendo huu matumizi ya nguvu kazi yatazidi kupungua kwa kasi. Je, unafikiria kutumia njia hiyo mbadala kwenye shamba lako?
Vyanzo: AirSeed, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.