fbpx

apps, Maujanja, sms, Teknolojia

RCS, Google waanza kusambaza teknolojia mpya ya SMS

rcs-google-waanza-kusambaza-teknolojia-mpya-ya-sms

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Google wameanza kusambaza teknolojia mpya ya SMS yenye lengo la kuwa ndio teknolojia ya kuacha na ile iliyozoeleka kwa miaka mingi katika huduma ya ujumbe mfupi (sms).

google playstore clubs bar

Katika kipindi cha zaidi ya mwaka na nusu kampuni ya Google imekuwa ikifanya mazungumzo na makampuni ya mitandao ya simu nchini Marekani juu ya uamuzi wake wa kutaka teknolojia mpya ya RCS iwe ndio teknolojia inayotumika kwa huduma za SMS. Ila imeonakana mitandao ya simu imekuwa kikwazo katika suala la kufanya maamuzi.

SOMA PIA  Je, Free Basics Ni sawa?

Teknolojia ya SMS ya RCS ipoje?

Teknolojia hii inawezesha app ya kawaida katika simu za Android kuweza kuwa na uwezo wa;

  • Taarifa za ujumbe kuwa umesomwa au hapana
  • Uwezo wa kujua kama mwingine anaandika muda huo
  • Uwezo wa kuwa na makundi kwa urahisi (Groups)

Google walikuwa na lengo la kuifanya teknolojia hii mpya ya SMS iwe ndio inayotumika kwa muda mrefu tuu. Katika mpango wao wa mwanzo walilenga kuhusisha mitandao ya simu katika utengekelezaji huo.

SOMA PIA  Call Recorder ACR: Ijue app ya kurekodi mazungumzo katika simu

Ila kutokana na hali ya kutopata ushirikiano mzuri, Google wameamua kuiwezesha teknolojia hiyo kwenye simu zake za Android bila kuishirikisha mitandao ya simu.

Mkurugenzi wa huduma za SMS wa Android, Bwana Sanaz Ahari, alipoulizwa ni lini huduma hiyo itasambaa kwa watumiaji wengine wa Android nje ya Marekani amesema tuwe tayari. Muda wowote wataanza na usambazaji wa teknolojia hiyo kwa nchi zingine.

SOMA PIA  Chrome 74: Jinsi ya kuweka muonekano wa giza kwenye simu/kompyuta

Lengo la Google ni kuhakikisha wanawezesha app ya kawaida ya huduma ya kuchati katika simu za Android kuwa na uwezo mbalimbali wa kitofauti wa kuweza kushindana na apps zingine kama vile WhatsApp.

Vipi je una mtazamo gani kuhusu teknolojia hii?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza
Tags: , ,

Comrade Mokiwa

Comrade MokiwaMuanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COMMuda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.| mhariri@teknokona.com |