fbpx
Ndege, Teknolojia, Usafiri

Boeing wasimamisha utengenezaji wa ndege za 737 Max

boeing-wasimamisha-utengenezaji-wa-ndege-za-737-max
Sambaza

Kampuni ya Boeing imesimamisha utengenezaji wa ndege za 737 Max. Kampuni hiyo imesema kuanzia Januari mwaka 2020 itaacha shughuli zote za utengenezaji wa ndege hiyo ilipigwa marufuku kufanya kazi duniani kote baada ya ajali mbili zilizotokana na matatizo ya kiufundi.

Ndege ya familia ya Boeing 737 Max ilikuwa tayari ndio ndege inayouza sana kwa sasa kutoka kampuni hiyo. Ajali ya kwanza ilikuwa ya ndege ya kampuni ya Lion Air iliyodondoka baharini – Java Sea Oktoba mwaka 2018, wakati bado uchunguzi ukiwa unaendelea ndege ya Ethiopian Airlines nayo ikadondoka ghafla Addis Ababa mwezi Machi mwaka 2019.

INAYOHUSIANA  Mkongo mpya wa mawasiliano chini ya bahari kuja Afrika Mashariki
airbus boeing
Watafiti wanaona Boeing walifanya haraka katika utengenezaji wa ndege hizi bila utafiti wa kutosha kiusalama. Walikuwa na haraka ili waweze kuleta ndege ya kushindana na ndege isiyotumia mafuta mengi kutoka Airbus, A320 Neo.

Ndege hizo mbili zimeua watu 346. Baada ya ajali hizi mbili vyombo vya usimamizi wa safari za anga duniani kote zilipata wasiwasi wa kuendelea kuacha ndege hizo kuendelea kufanya kazi kabla ya uchunguzi mkubwa. Hadi sasa uchunguzi unaonesha kampuni hiyo ilifanya utengenezaji wa haraka ambao haukuzingatia baadhi ya mambo ya kiusalama. Pia hakukuwa na mafunzo mazuri kwa marubani juu ya teknolojia mpya za kwenye ndege hizo zilizokuwa na uwezo wa kumpokonya rubani uwezo wa kufanya mabadiliko ya kiundeshaji dhidi ya progamu ya kompyuta.

INAYOHUSIANA  Ushindani katika vioo vinavyojikunja

Kwa muda mrefu kampuni ya Boeing imeamini baada ya kufanya mabadiliko na maboresho (yaliyohusisha mabadiliko katika programu ya kompyuta ya kwenye ndege hizo – na hivyo rubani kupewa kipaumbele katika maamuzi ambayo mwanzo programu ya kompyuta ndio ilikuwa juu) basi wangewahi kuruhusiwa kuendelea na mauzo na wateja wao kuendelea kutumia ndege hiyo.

Chombo cha usalama wa anga cha Marekani, tayari kimesema bado hakijaridhisha kuhuruhusu ndege hizo kurudi kazini hivi karibuni.

ndege za 737 max
Ndege za 737 Max zikiwa zimechukua nafasi ya eneo la maegesho ya magari ya wafanyakazi wa Boeing. Bila uwezo wa kuzipeleka kwa wateja wake ndege hizo zimekwama kuondoka kiwandani.

Hadi sasa kampuni ya Boeing ina takribani ndege mia 400 za Max 737 zilizokaa kwenye viwanda vyake tayari kwa kupelekwa kwa wateja. Kama ndege hiyo ikakataliwa moja kwa moja basi itakuwa ni moja ya hasara kubwa zaidi kuwahi kupatikana katika sekta hiyo.

INAYOHUSIANA  Bluetooth 5.0 - Kasi ya mara 2 zaidi, umbali wa mara 4 na ukubwa wa mafaili wa 800% zaidi

Kwa kampuni ya inayoshindana na Boeing, Airbus hiki kimekuwa kipindi ambacho ndege yao inayoshindana moja kwa moja na Max 737, ndege ya 320 neo kuendelea kuangaliwa kama chaguo bora kwa mashirika ya ndege yanayotaka kununua ndege mpya.

Vyanzo: CNN na tovuti mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |