Dunia ya leo ni ya ushindani ambayo inapata msukumo mkubwa kutokana na ukuaji wa teknolojia unaopanuka kila sekunde. Washindani wa karibu sana kwa Apple kwenye biashara, Google wapo njiani kutoa Google Pay katika mfumo wa kadi.
Si dhambi kuiga kitu kizuri 😀 😀 ambacho kitakuweka katika nafasi nzuri ya kuvutia watu hivyo basi kuweza kupata wateja wengi (wapya na wa zamani) kulingana na kile ambacho kinaweza kufanyika kwa kutumia bidhaa hiyo ambayo imeingia sokoni.
Google Pay ni nini?
Hii ni kadi ya kufanya malipo iliyotengenezwa na Google ambayo inakuwa imeunganishwa na akaunti yako ya benki itakayokuwezesha mteja kuweza kufanya malipo ya bidhaa kwa njia ya kidijiti hata kama ana salio (pesa) pungufu kisha kulipa deni wakati mwingine.
Kadi hiyo imeshafanya makubaliano ya kibiashara na Mastercard, VISA pamoja na benki mbalimbali kurahisisha miamala kuweza kufanyika kiurahisi. Vilevile, Google Pay kwa sasa inamuwezesha mteja kuweza kufanya malipo mtandaoni bila shida yoyote lakini pia kumpa uwezo mtu kuifunga/kuzuia muamala ambao unatia shaka.
Uamuzi wa ujio wa kadi hiyo tafsiri ni kuendelea kuleta ushindani wa karibu kabisa kwa wapinzani wenzao ambao tayari wana Apple Card tangu Agosti 2019 lakini tofauti yao kubwa ikiwa kiasi ambacho mteja anaweza kutumia kufanya malipo ya bidhaa.
Vyanzo: MacRumors, GSMArena