iPhone Hizi Ndio Zinazokubali Teknolojia Ya “Wireless Charging”!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ni wazi kuwa teknolojia za kuchaji simu zetu ni nyingi sana siku hizi. Ukiachana na ile ya kawaida ambayo imezoeleka na wengi wetu  kuna nyingine inayojulikana kama ‘wireless charging’, yaani uwezo wa kuchaji simu bila hata ya kuchomeka waya wa chaja moja kwa moja katika simu.

Sasa katika simu za iPhone je ni zipi ambazo zinakubali teknolojia hii? Leo teknokona inakuhabarisha kuhusiana na jambo hili maana tumepata ombi la kuwahabarisha wasomaji wetu juu ya jambo hili.

  • iPhone 11 Pro Max (2019)
  • iPhone 11 Pro (2019)
  • iPhone 11 (2019)
  • iPhone XR (2018)
  • iPhone XS Max (2018)
  • iPhone XS (2018)
  • iPhone X (2017)
  • iPhone 8 Plus (2017)
  • iPhone 8 (2017)

Pengine matoleo ya juu zaidi (yajayo) yanaweza au yakawa na uwezo mkubwa wa kuja na teknolojia hii.

Wireless Charger

Wireless Charger Ikiwa Inachaji iPhone

Kingine kizuri ni kwamba simu zore hapo juu zinakubali teknolojia ya ‘Fast Charging‘ pia. Kuna mambo mambo yanaweza kujitokeza wakati unatumia teknolojia hii (sio lazima yatokee), chini ni baadhi ya mambo na hatua za kuchukua endapo yakitokea

INAYOHUSIANA  eSIM: Teknolojia ambayo haijaenea sana

MUHIMU

iPhone hata kama inakubali teknolojia hii haitaweza kuchaji kama ukiwa umeiunganisha moja moja na chaja ya kawaida au USB. kwa kifupi unaweza kuchaji kwa kutumia chanzo kimoja kwa muda husika.

Jitahidi kuweka ‘Do not Disturb’ ili kufanya simu kuwa kimya maana baadhi ya ‘notification’ za ujumbe mfupi na mitandao ya kijamii zinasababisha simu kunguruma (vibrate) hii inaweza sababisha simu yako kuhama katika eneo lake la kuchajia.

Wireless Charger

Vile vile simu  inaweza onyesha hali ya kupata hali ujoto joto ambao sio wa kawadia. Ujoto joto huu unaweza kuwa unasababishwa na koili ndani ya ‘wireless charger’ na simu hazijarandana vizuri. Sasa ili kuepukana na hili inabidi haili hii ikitokea, uache kuchaji simu yako kwa muda au uende kuchajia katika eneo ambao ni tulivu na lenye ubaridi ubaridi (sio ubaridi kama wa jokofu) mfano karibia na feni.

INAYOHUSIANA  Tim Cook wa Apple asema “Najivunia Kuwa Shoga”

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la maoni. Je hapo mwanzo ulikuaunafikiria ni simu gani za iPhone zinakubali teknolojia ya kuchaji bila kuchomeka nyaya katika simu hizo?

Tembelea TeknoKona kila siku kwani daima tupo nawe katika sayansi na teknolojia kwa ujumla.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.