Ndege ya Boeing 737 MAX 8 ni ndege maarufu sana kwa sasa, lakini si kwa umaarufu mzuri. Ndege ya aina hii ndiyo iliyopata ajari majuzi na kuua abiria na wafanyakazi wote waliokuwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Ethiopia.
Kwa kifupi hii ni ajali ya mbili ya ndege hiyo hiyo kutokea katika kipindi cha chini ya miezi 6 – na kibaya zaidi ni kwamba ni ndege mpya kabisa na kwa ajali mbili katika kipindi cha miezi 6 kwa ndege za familia mpya ni kitu ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya ndege za biashara.
Kwa sasa kuna takribani ndege 350 za Boeing 737 MAX 8 duniani kote, zikimilikiwa na mashirika 54 ya ndege.
Historia
Ndege za familia ya Boeing 737 zilianza kutengenezwa mwaka 1966 huko nchini Marekani, ndege ya kwanza kupaa kwa majaribio ilifanya hivyo tarehe 9 Aprili 1967.
Ndege hizi zinatengenezwa mahususi kwa ajili ya safari fupi na zile za masafa ya kati. Kwenye biashara ya ndege huwa umbali unawekwa kimakundi haya;
Masafa ya kati ni umbali unaocheza katikati ya masafa mafupi na marefu. Vipimo hivi vinatofautiana kati ya shirika moja la ndege hadi jingine, hapa tumekupa wastani tuu kulingana na data za Wikipedia.
Sifa moja kuu ya muonekano wa ndani wa familia hizi za ndege ni uwepo wa korido moja tuu, yaani eneo linalotenganisha viti vya abiria kushoto na kulia. Kiutendaji ni kwamba zinatengenezwa huku zikihakikisha utumiaji wa mafuta unakuwa mdogo zaidi kwa ajili ya biashara za ndege ziweze kutengeneza faida kwa safari zisizo za umbari mrefu sana.
Muonekano wa ndani wa Boeing 737 Max 8 ya Shirika la ndege la Ethiopia
Ndege ya Boeing 737 MAX 8 inakuja na viti kati 162 hadi 178 kulingana na mahitaji ya mteja. Ingawa wenyewe wanasema ina uwezo wa kuwa na viti 200. Imetengenezwa ikiwa na uwezo wa kutumia mafuta chini zaidi kwa asilimia 20 ukilinganisha na ndege zingine za familia ya 737.
Umbo la injini zake limetengenezwa mahususi kwa ajili ya kusaidia kupunguza kelele za ingini.
Toleo hili ni moja ya toleo linalofanya vizuri zaidi kimauzo kwa Boeing, shirika la utengenezaji ndege la Marekani. Kufikia Januari mwaka huu Boeing ishauza ndege 350 za Boeing 737 Max 8 na tayari ina oda ya ndege zingine 5,000 (Ndege ya kwanza kujaribiwa baada matengenezo ilifanyiwa majaribio mwezi Januari mwaka 2016, na mwezi Mei mwaka 2017 ndiyo ndege ya kwanza ya Boeing 737 Max 8 ilipelekwa kwa mteja.
Jinsi ajali mbili zilivyotokea kuna hali ya kufanana kubwa inaonekana, zote zilidondoka dakika chache baada ya kuruka. Watafiti wa mambo wengi wanaona mfumo wa kompyuta wa kuhakikisha ndege haikai kwenye hali ya kudondoka ndio utakuwa una makosa. Kwa sasa bado uchunguzi unaendelea kwani kifaa maarufu kwa jina la Boksi Jeusi (Black Box) kimeshapatikana.
Boeing 737 Max 8 ya shirika la Ethiopian Airways
Tayari mataifa mbalimbali yamepiga marufuku ndege hizo kutumika hadi watakapojiridhisha, nchi hizo ni pamoja na Uchina, Indonesia, Ethiopia.
Kwenye soko la hisa, hisa za Boeing zimedondoka kwa asilimia 22.53 kufikia leo asubuhi (12-03-2019). Na tayari abiria wengi wa ndege wameonesha nia ya kukagua aina za ndege kabla ya kukata tiketi za ndege, wengi wakitaka kutopanda ndege ya 737 Max 8 hadi hapo uchunguzi ukikamilika.
Boeing 737 MAX 8 kwa ufupi;
Oda 5,011 (Januari 2019)
350 zishapelekwa kwa wateja
2 zimeshaanguka
189 – idadi ya watu walifariki kwenye ajali Lion Air crash (Oktoba 2018)
157 – idadi ya watu waliofariki kwenye Ethiopian Airlines (Machi 2019)
114 idadi ya ndege za Max 8 zilizopigwa marufuku kutumika baada ya ajali ya Ethiopian Airlines. (97 China, 4 Ethiopia, 1 Garuda, 10 Lion Air na 2 Cayman)
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Mbunifu na mpenda teknolojia.
Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM
Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.
| mhariri(at)teknokona.co.tz |