fbpx
Android, apps, whatsapp

WhatsApp kuacha kufanya kazi katika simu hizi mwaka 2020

whatsapp-kuacha-kufanya-kazi-simu-mwaka-2020
Sambaza

WhatsApp kuacha kufanya kazi katika mamilioni ya simu kuanzia mwaka 2020. Simu hizi ni matoleo ya nyuma ya simu zinazotumia Android, iOS na Windows Phone.

whatsapp app WhatsApp kuacha kufanya kazi
WhatsApp kuacha kufanya kazi: Je simu yako itaendelea kuwa na sifa?

Kampuni ya WhatsApp inayomilikiwa na Facebook imetoa taarifa ikisema inasikitika na uamuzi huu ila ni uamuzi wa kilazima kufanyika ili kuhakikisha wanaendelea kuwa na uwezo wa kuhakikisha watumiaji wake wanakuwa salama dhidi ya udukuzi ambao unaweza kufanywa kwenye matoleo ya nyuma ya programu endeshaji za simu.

Kwa watumiaji wa simu zenye sifa zifuatazo wajiandae kuona app ya WhatsApp ikisumbua kufanya kazi ifikapo Februari 1 2020, kama simu zao zinauwezo wa kupokea matoleo mapya ya programu endeshaji basi wanashauriwa kufanya hivyo.

INAYOHUSIANA  Jinsi ya Kupakia WhatsApp yenye Ladha Tofauti kwenye Simu yako

Unatumia iPhone 5

Simu za iPhone 5 na 5S kutoka Apple zinaonekana kuwa ni baadhi maarufu ambazo zitaathirika kwa uamuzi huu. Bado zinatumika hasa kwa mataifa yanayoendelea. Tovuti ya DeviceAtlas ilisema kufikia mwaka huu simu za iPhone 5 na 5S zinawakilisha zaidi ya asilimia moja na nusu ya simu zinazitembelea tovuti mbalimbali mwaka huu.

  • Android – Kwa android ni kwa simu zinazotumia programu endeshaji ya 2.3.3 Gingerbread na kurudi nyuma. Kama unatumia simu yeyote ya Android (mfano kutoka Samsung, Huawei, Sony na Google) iliyotoka ndani ya kipindi cha miaka 10 iliyopita utakuwa salama.
  • iOS (iPhone) – Kwa simu za iPhone toleo lolote la programu endeshaji la iOS kuanzia la 8 kwenda nyuma hazitakuwa na sifa tena. iOS 8 ni programu endeshaji iliyotambulishwa mwaka 2014. Simu ya chini kabisa yenye sifa ya kupokea toleo la iOS la kisasa zaidi la iOS 8 ni simu ya iPhone 6. Hii inamaanisha kama unamiliki iPhone yeyote iliyotoka kabla ya iPhone 6 basi ujiandae app hiyo kutoweza kufanya kazi tena ifikapo Februari 1, 2020.
  • Windows Phones – Simu zote zinazotumia toleo la Windows 8.1 au lolote jipya ndio wataendelea kuwa na uwezo wa kutumia WhatsApp. Matoleo ya nyuma yake haitawezekana tena.
INAYOHUSIANA  Gallery Go ndio mbadala wa Google Photos

Je una mtazamo gani kuhusu maamuzi haya kutoka WhatsApp? Je simu yako bado ina sifa?

Chanzo: WhatsApp Blog
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |