BlackBerry ni jina lenye hishima kubwa na na kampuni mbili hadi sasa kwa nyakati tofauti zimeshainunua na kutaka kutoa bidhaa mpya ambazo zinabeba jina hilo lakini zimekuwepo changamoto nyingi ambazo zimesababisha mipango ya ujio mpya kutokwenda sawia.
Hivi karibuni tuliandika kuhusu OnwardMobility kutaka kurudisha kwenye ramani simu jana za BlackBerry hasa wakiwa wamejipanga kuja na kicharazio/rununu ambayo inakubali teknolojia ya 5G na tulieleza mengi zaidi humo lakini sasa suala hilo limewekwa kampini na tusitegemee ujio wa Blackberry ya 5G.
Kwa mujibu wa taarifa waliyotoa OnwardMobility kupitia tovuti yao wanasema ni kwa huzuni kubwa wanaacha biashara na hata kutengeneza simu janja yenye ulinzi wa hali ya juu ikiwa na kicharazio.
Taarifa hii inaweza isiwe ya kushtusha sana kwani zilikuwepo taarifa kuwa mpango wa OnwardMobility kuja na simu janja (BlackBerry) inayitumia teknolojia ya 5G umesitishwa lakini wengi hawafahamu kilichosababisha kufikia hatua hiyo. Hata hivyo, iliaminika huenda OnwardMobility wakatoa kicharazio ambacho kinaweza kutumia kwenye simu za Android na teknolojia ya 5G bila ya kuwa na jina-BlackBerry.
:format(webp)/cdn.vox-cdn.com/uploads/chorus_image/image/70535754/verge-2015-11-06_15-38-09.0.0.jpg)
Haifahamiki sababu ya kilichowafanya OnwardMobility kuachana na kutengenza simu janja za BlackBerry lakini pia kufunga kabisa kiwanda ingawa kwa habari za chini kwa chini kutoka kwa Android Police inaonekana leseni ya kutumia jina-BlackBerry ilisitishwa kutumika hivi karibuni na mbali na hiyo sio rahisi kuendelea na utengenezaji wa simu janja kwa kampuni inayochipukia katikati ya janja la uhaba wa vipuri mama.
Haya sasa kama tulikuwa na shauku ya kuona toleo jipya la BlackBerry inabidi tuwe wapole na tufikirie mambo mengine kwani hali imebadilika, kilichotegemewa hakijatimia na wahusika wamekubali yaishe!
Vyanzo: The Verge, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.