fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Maujanja simu

Mambo 3 Ambayo Inabidi Kila Mwenye Simu ya Android Ayafahamu! #Maujanja

Mambo 3 Ambayo Inabidi Kila Mwenye Simu ya Android Ayafahamu! #Maujanja

Spread the love

Ni sawa kabisa kuwa vifaa vya Android huwa vinakuja na mambo mengi mazuri ndani yake. Ukiachana na vipengele vya kawaida ambavyo karibia kila mtu mwenye simu ya Android anavijua kuna vile ambavyo kidogo havijulikani kwa kiasi kikubwa…usijali leo tutakuonyesha vitu 3 muhimu sana kufahamu!

Kufahamu mambo haya itakusaidia kuweza kutumia kifaa chako kwa ufanisi zaidi, kulinda usalama wa data zako bila ya kusahau kuwa na utumizi mzuri wa betri la kifaa chako cha Android

> Punguza manjonjo ya Animation – Okoa chaji na ufanisi wa simu

android animation

Sawa wengine wanaweza kataa kufanya hivyo kwani wanaona kama vifaa vyao vinapoteza muonekano wake mzuri. Sawa ni kitu kizuri kuwa nacho lakini kwa kiasi kikubwa kinashusha ufanisi wa kifaa chako katika kufanya kazi yake kama inavyotakiwa.

Ili kupunguza Animation nenda katika Settings >> Developer Options >> Window animation Scale. hapo unaweza ukawa umepoteza ule mwonekano wako mzuri lakini nakuhakikishia kwamba utakuwa umeoneza kiasi cha ufanisi na hii ni kujumuisha na spidi katika simu yako .
Unaweza ukapunguza kiwango cha Animation mpaka 0.5X au unaweza amua kuizima kabisa ingawa ni vizuri zaidi kuipunguza tuu.

> Desktop Backup Password – Zuia kuibiwa data kwa USB

Kila mmoja wetu ana tarifa zake za muhimu kama vile zile za kibenki, picha zile ambazo ni siri yako na mengine mengi ya siri katika simu yako. Na pia kumbuka hatutaka mtu aweze kuchukua Data za kwenye simu hii kwa kuunganisha na waya wa USB kwenye kompyuta.
Ili kuzuia aina hii ya wizi Android wana kipengele mahususi ambacho kinaweza kukusaidia katika hili. Unaweza weka nenosiri (password) kwa ajili ya ulinzi. Ulinzi huu utakuwa pale unapochomeka USB ili kuweza kuona mafaili yaliyopo katika kifaa kwa kutumia kompyuta basi itakulazimu uingize Nenosiri (password).

Ili kuliwezesha hili nenda katika Settings >> Developer Options >> Desktop Backup Password .Katika kifaa chako cha Android  Kitu kingine katika vifaa vyetu vya Android ni Background Data

> Zuia Baadhi Ya Taarifa Nyuma Ya Pazia – Utumiaji wa data (intaneti)

Wengi wetu tunalalamika sana kuwa simu zetu hazikai na chaji na MB/GB zinaisha kimazingara. Ubaya wa chaji ya simu na hata bando ni kwamba huwa zinalika hata kwa zile App ambazo hatuzitumii muda huo ambazo zinajiendesha kwa siri nyuma ya pazia.

SOMA PIA  Usalama wa nywila kwenye simu yako unatokana na ushikaji wa simu

utumiaji data mwenye simu ya android

Lakini kumbuka una uwezo wa kuzizuia App hizo kula Data zako au hata kuzifanya kula kidogo. Ili kuwezesha hilo nenda katika Settings >> Data Usage.
Ukiingia hapo utaona kiwango cha data kinacholiwa na kila App katika simu yako. Hapo unaweza ukaamua kukataza App ambazo huzitumii mara kwa mara kuweza kula Data.

Mpaka hapo umepata darasa tosha sio? Niandikie sehemu ya comment ni nini pia unahisi ni kizuri na kinafaa kujulikana kwa wengine katika vifaa vyetu vya Android!

Pia kama ungependa TeknoKona iandike kuhusu kitu Fulani mwagika sehemu ya comment hapo chini pia. Kumbuka TeknoKona siku zote tupo nawe katika masuala ya teknolojia!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania