Tumekuwa tukiulizwa mara nyingi na wasomaji wetu maswali kuhusu anti- virus katika simu za Android, wapo ambao wanataka kujua pengine ni app gani nzuri kutumia kama anti-virus katika simu za Android pia wapo wachache ambao wamekwenda ndani zaidi na kuuliaza kama kuna ulazima wa kutumia anti-virus katika simu za Android.
Makala hii inajadili kiundani kama kuna ulazima wa kutumia anti-virus katika simu za Android.
Soma Pia – Njia za kupata Data zako zilizopotea (zilizofutwa) kwenye simu ya Android
Katika dunia ya sasa ambayo matumizi ya simu yamekuwa makubwa na yakienda sambamba na kasi ya udukuzi na uhalifu wa mitandao swala la usalama hatuwezi kulifumbia macho ama kulichukulia urahisi. Wengi wameingia katika matatizo makubwa baada ya kuwapa mwanya wahalifu wa kimtandao hivyo ni wajibu wa kila mtumiaji wa simu kuhakikisha kwamba yupo salama dhidi ya uhalifu wa kimtandao.
Kimsingi simu yeyote ya Android ambayo ina mpangilio halisi inapewa uwezo wa kuzikubali tuu app zote ambazo zinapatikana katika PlayStore ya Google na kukataa app yeyote inayotaka kupakuliwa kutumia njia nyingine ambayo kwa namna moja ama nyingine inaweza kuruhusu virusi ama kutoa mwanya kwa wadukuzi kuweza kuishambulia simu yako.
Google wenyewe pia wanafanya jitihada kubwa katika kuhakikisha apps zinazowekwa kwenye soko lao ni salama na ndio maana hawashauri mtu kupata apps kwa njia nyingine kutoka sehemu ambazo si salama.
Hii inamaana kwamba kama simu yako wewe haijachokonolewa yaani haijafanyiwa mabadiliko yeyote yatakayo ruhusu app ambazo hazijakaguliwa na Google kuingia katika simu yako basi hautahitaji kuwa na app ya anti-virus katika simu yako.
Ikumbukwe kwamba kila mtu anamatumizi yake ya simu, hii inaweza kusababisha baadhi yetu wakawa wanahitaji mfumo wa ziada wa ulinzi hii sio mbaya na haina shida ila sio muhimu.
Mimi binafsi situmii kabisa app ya anti-virus katika simu za Android ambazo ninazimiliki hii ni kwa sababu mimi nina matumizi ya kawaida, ukiniomba ushauri juu ya kutumia ama kutotumia app ya anti-virus katika simu za Android nitakushauri kadiri ya matumizi yako ya simu kwa matumizi ya kawaida nisingekushauri kutumia app yeyote maana Android inajitosheleza.
Hata mkuu wa usalama wa Android Ludwig mwanzoni mwaka huu alisema kwamba asilimia 99 ya watu wanaotumia app za anti-virus katika simu za Android hawana wanachonufaika na app hizo kwa maana kwamba kazi kubwa inakuwa imekwisha fanywa na hatua za kiusalama za Android.
Tuambie je ulikuwa unatumia anti-virusi? ulikuwa unajua kama Android wanakulinda dhidi ya virusi? naje utaendelea kutumia huduma hizi ama utaachana nazo ama bado utaendelea kutumia.
Soma Pia – Njia za kupata Data zako zilizopotea (zilizofutwa) kwenye simu ya Android
One Comment
Comments are closed.