fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Kwanini Hisa za Twitter zinazidi kuanguka.?

Kwanini Hisa za Twitter zinazidi kuanguka.?

Spread the love

Mtandao wa Twitter umefanya mambo mengi sana katika jitihada zake za kuzifanya hisa zake ziweze kupanda bei sokoni, lakini kinyume na jitihada za mtandao huu hisa zake sokoni zimekuwa zikiporomoka kila uchao mfano wa gari bovu katika mteremko mwanana.

Tangu siku ya kwanza ambapo Twitter iliandikishwa katika soko la hisa nchini marekani hisa zake zimekuwa zikishuka na kushuka kitu ambacho kwa tafakari ya haraka ni kwamba wawekezaji wanaona kwamba biashara hii haina faida lakini kwa jicho la mbali hii inamaana kwamba pengine mtandao huu hautakuwepo miaka mingi baadae.

Pengine unawaza ni kwanini Twitter wanashindwa kufanya vizuri katika soko kama ilivyo kwa mitandao mingine ya kijamii kama Facebook, katika makala hii nitajaribu kuonesha baadhi ya sababu ambazo zimepelekea mtandao huu kuwa hapa ulipo sasa pia nitajadili yale ambayo Twitter imefanya kujaribu kunusuru bei za hisa zake.

Twitter ni mtandao mgumu kutumia

Tofauti na mitandao kama Facebook ambayo ni rafiki na watumiaji ni rahisi kuwa mwenyeji haraka, Twitter imekuwa ni ngumu kidogo kwa watumiaji wapya. Sio kitu kigumu kukutana na mtu akakwambia kwamba alishindwa kuuelewa mtandao huu unavyofanya kazi.

SOMA PIA  Makanisa kuwekwa Wi-Fi nchini Ujerumani

Kimsingi hii ndiyo sababu kuu ya kushindwa kwa mtandao huu katika soko, inachangia kwa Twitter kuwa na watumiaji walio hai wachache ambao wanaongezeka kila siku hii inasababisha isiwe inapata  matangazo ya kutosha (ambayo yangeleta mapato makubwa) na hivyo thamani ya hisa zake kushuka.

Twitter ni jeshi la mtu mmoja

Ndio Twitter inategemea watumiaji wa App yake kuu tu kwa ajiri ya kutengeneza wigo wa matangazo ya mtandaoni ambayo ndiyo chanzo kikuu cha mapato kinachokuza thamani ya hisa, wakati mtandao kama Facebook unakusanya watumiaji kutoka Facebook na pia kutoka katika app yake ya Instagram ambayo inafanya vizuri katika mitandao ya kijamii. Facebook imefanikiwa kumiliki apps nyingine kubwa zinazofanya vizuri na hivyo kuzidi kuipa hadhi zaidi.

Twitter wamekuwa wanachelewa kufanya maamuzi ya muhimu.

Mtandao huu umekuwa ukichelewa kufanya maamuzi ama mabadiliko ya maana kila wakati yanapohitajika na hii imekuwa ikiigharimu kampuni hii kibiashara. Kwanza ni kuchelewa kubadilisha mfumo wa uendeshaji wake wakati ilipoanza ili kuweza kutengeneza mapato makubwa zaidi ( Twitter ilipoanza ilikuwa katika muundo ambao haukuwa umekaa kiukusanyaji wa mapato zaidi).

SOMA PIA  Jacquard: Jaketi janja kutoka Google na Levi's

Pili  Twitter walichelewa kumuweka Jack Dorsey katika nafasi ya Utendanji mkuu baada ya hatua za kumtoa Dick Costolo  kufanikiwa ili Jack Dorsey aingie katika nafasi hiyo na kufanya mabadiliko ambayo yalikuwa yakihitajika.

Hisa za Twitter

Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter Jack Dorsey

Wataalamu wa mambo wanasema kwamba hisa za Twitter zitazidi kushuka mpaka pale kampuni hii itakapopata namna ya kuwavutia watumiaji wengi wapya ambapo kufanya hivi pengine kutasababisha watumiji wengi ambao wapo hai sasa hivi kuihama Twitter.

Hivyo uhai wa Twitter miaka ijayo umekuwa kama kitendawili kwa sasa kutokana na ukweli kwamba hakuna anayejua njia gani itachukuliwa na wamiliki.

Comment

Comments

  1. […] ambayo imekuwa katika nyakati ngumu baada ya hisa zake kutokuwa zinafanya vizuri katika soko imekuwa katika jitahada za kila namna za kuongeza watumiaji hai, hii ni karata nyingine […]

  2. […] Soma zaidi: Kwanini hisa za Twitter zinazidi kuanguka sokoni […]

TeknoKona Teknolojia Tanzania