fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Infinix simu Teknolojia

Hizi ndio sifa za simu janja Infinix Note 10 Pro

Hizi ndio sifa za simu janja Infinix Note 10 Pro

Spread the love

Kwa miaka kadhaa sasa Infinix wamekuwa wakiendelea kutoa simu janja ambazo ni mwendelezo wa familia ya “Note” ambapo miezi kadhaa ilitoka Infinix Note 10 Pro.

Familia ya Infinix Note imekuwa ikishindana kwa karibu sana na simu janja za Samsung Note lakini kila moja inajitofautisha kwa namna yake na mwisho wa siku sisi wateja ndio tunatoa hukumu ya mwisho kwa maana ipi imenunulika zaidi kuliko nyingine. Leo hii Infinix imetokea kullivutia jicho langu kutokana na sababu mbalimbali. Simu hii ina sifa zifuatazo:-

Memori :
 • Diski uhifadhi: 64GB/128GB/256GB+sehemu ya kuweka memori ya ziada
 • RAM: GB 6/8
Betri/Chaji :
 • Li-Ion 5000 mAh
 • USB-C 2.0, OTG+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 33W
  Infinix Note 10 Pro

  Simu hii ina teknolojia ya 4G LTE, inatumia kadi mbili za simu. Teknolojia ya kutumia alama ya kidole imewekwa kwa pembeni(kwenye kitufe cha kuzima/kuwasha simu), inatumia Bluetooth 5.0, WiFi.

   

Kipuri mama :
 • MediaTek Helio G95
Uzito :
 • Gramu 209

Programu Endeshi

 • XOS 7.6, Android 11
Rangi :
 • Zambarau, Nyeusi na Bluu mpauko

  Infinix Note 10 Pro

  Infinix Note 10 Pro ina redio, sehemu ya kuchomeka spika za masikioni

Simu hii imeingia tangu mwezi Juni mwaka huu na bei yake inaanzia Tsh. 600,000 kwenye maduka ya Tigo Tanzania. Kumbuka kufuatilia TeknoKona ili uweze kuhabarika halikadhalika kuelimika kuhusu teknolojia.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania